Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,310
Kasisi John Chilembwe alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kibaptisti na mpigania uhuru wa Malawi, ikiitwa Nyasaland na ikikaliwa kimabavu na Uingereza, aliyeishi kati ya mwaka 1871 na 1915.
Vyanzo tofauti vinataja asili tofauti ya Chilembwe, mtaalamu mmoja, Joseph Booth akimhusisha na kabila la Wayao ambalo hupatikana Kaskazini mwa Malawi, Kaskazini MAgharibi mwa Msumbiji na Kusini mwa Tanzania.
Chilembwe alipata elimu yake ya Biblia na Ukasisi huko Marekani, kabla ya kurejea Malawi na kujiunga na vuguvugu la harakati za kuowaondoa madhalimu wa Kiingereza, akitumia Kanisa kama sehemu yake ya ushawishi.
Mara tu baada ya kuanza kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Chilembwe alijaribu bila mafanikio kuanzisha vuguvugu la kuuondoa utawala wa Waingereza, Kasisi huyu anatajwa kuwa miongoni mwa Wapigania Uhuru wa kwanza kabisa Barani Afrika.
Moja ya Falsafa iliyomtangaza sana Chilembwe ni ie iliyohoji uhalali wa Yesu kuwa mtu mweupe, akidai kuwa kuna ulazima wa kuwa na Yesu, mkombozi na mwokozi ambaye ni miongoni mwa watu wetu, ni kama kusema kuwa Chilembwe alikuwa anajaribu kuchukua nafasi ya Yesu.
Upinzani kutoka Serikali Dhalimu ya Waingereza ulikuwa ni mkubwa wakati wa harakati za Chilembwe, ikiwemo kupitisha sheria za kuwanyonga watu weusi ambao walijihusisha na harakati hizo, sheria za Martial ambazo hata hivyo zilikuja kufeli baadae.
Kauli Mbiu ya harakati za Chilembwe ilikuwa ni 'Afrika kwa ajili ya Waafrika', ikilenga kutimizwa matakwa ya kisiasa zaidi kulio ya kidini kama yalivyokuwa malengo ya taasisi yake.
Mwaka 1914, Chilembwe aliandika Barua kali kwenda kwa Mhariri wa Gazeti la Nyasatimes, akipinga kuhusishwa kwa Waafrika kwenye Mapmbano ya Karonga kati ya Serikali za Ujerumani (Tanganyika) na Uingereza akidai kuwa idadi ya Waafrika waliokufa ni kubwa, na bila sababu.
Chilembwe na wapiganaji wengine waliuwawa kwenye Mapambano ya Januari - Februari 1915 kwenye vilima vya Shire, tarehe ya kufa kwake ikirekodiwa kuwa Februari 3 1915.
Baada ya Uhuru mwaka 1964, Chilembwe akatambuliwa kama Mpigania Uhuru na Shujaa wa Taifa, huku Mfano wa Sura Yake ukionekana kwenye noti zote za nchi hiyo hadi mwaka 2012 Benki Kuu ya Malawi ilivyotoa noti mpya ambako hadi sasa uso wa Chilembwe ungali kwenye noti ya Kwacha500.
Tarehe 15 Januari, inaadhimishwa kama siku ya shujaa huyu nchini Malawi.
Imeandikwa kwa msaada wa Intaneti