DOKEZO Malalamiko: Wezesha portal - Dar Kariakoo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kwa niaba ya wafanyabioshara wa Kariakoo-Dar, kata ya Kariakoo, mtaa wa Kariakoo Magharibi, tunaomba mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mchakato wa usajiri na utoaji vyeti kwa vikundi vilivyo kidhi vigezo kulingana na taratibu husika kuchukua hatua dhidi wa Afisa Maendeleo- kata ya kariakoo, kwa kutotoa ushirikiano kwa wafanyabiashara hasa wanapotaka kupata elimu, kusidiwa ukaguzi wa nyaraka zao ili kupewa vyeti na kutambulika na mamlaka husika.

Afisa huyu, amekuwa mzito tangu zoezi lilipo anza, jambo linalopelekewa wananchi kuhamasishana wenyewe bila kuwa na mtu wa kuwaongoza, hata atakapotafutwa hayupo tayari kutoa ushirikiano, tukituma taarifa zetu za kuomba kusajiriwa inachukua wiki 3, mwezi hadi miezi kufanyiwa kazi, jambo ambalo linakatisha tamaa wanavikundi na kusambaratisha baada ya kuona kuna harufu ya utapeli na rushwa.

Tuna imani sana sana na Rais Samia kwa namna alivyolenga zoezi lili liwe bora, tunaimani sana na waziri wa tamisemi, mh Mchengerwa tunaimani nae sana ,ila watendaji wanaharibu zoezi hili na kuonekana kuwa ili kupitishwa kikundi ni mpaka utoe chochote, kwa wananchi hawaelewi kutopewa vyeti wakati hakuna sababu zinazo wekwa wazi, na hatupewi ushirikiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…