Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Taratibu zao za makusanyo,mapato na matumizi binafsi sizijui kwa undani ila kuna mambo huwa najiuliza sana kuhusu hizi taatifa zao za kila mwezi.Utoaji wa taarifa hizi kwa umma kwakweli ni jambo jema sana, hata hivyo kuna mambo naona yanahitaji ufafanuzi hapa.
Kwa mfano,anaekusanya ndio huyo huyo anaetangaza.Sina shida sana na hili ila naomba kujua makusanyo haya yanayotangazwa kila mwezi mimi mwananchi wa kawaida naweza kuyathibitisha vipi?
Alafu kama wanatoa matumizi ya makusanyo hayo kwa kila mwezi,ni nani anahakiki matumizi haya yamefanyika kama yalivyopangwa?
Kwa mfano, wanaposema mwezi huu tutalipa /tumelipa malimbikizo ya mishahara kiasi fulani,nani anahakiki malipo haya au ndio mpaka tusubiri ripoti ya CAG?Je,hii ni sahihi?Wakaguzi wa ndani kwanini nao wasiwe wanatupa taarifa zao za kila mwezi juu ya matumizi ya makusanyo haya?Kama tatizo ni sheria,kwanini tusibadili/ tusitunge sheria hizi sasa?
Alafu mbona kama hamna muda ambao ni fixed wa kutangaza makusanyo ya kila mwezi?Wanatangaza baada ya siku 28,29,30,31 au hata zaidi ya hapo?Najua kuna swala la week-end,lakini linaweza kuwa ndio sababu?
Kwa kuongezea katika hili,ni vizuri tukawa na chombo huru,ambacho pamoja na mambo mengine, kitakuwa na jukumu la kuthibitisha makusanya haya ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mchanganuo mzima wa mapato na matumizi ya fedha hizi.Chombo hiki pia kiwe na jukumu la kutoa feedback kwa umma juu ya matumizi haya kwa kila mwezi.