Makumbusho mia tatuuu !!!

Makumbusho mia tatuuu !!!

Padri Mcharo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2015
Posts
1,899
Reaction score
3,691
"Makumbusho mia tatuuu, makumbusho mia tatuuuu !!! Panda ukaeee"

Alisikika konda kwenye kituo cha Mwenge Mataa (mkabala na kiwanda cha Shellys Pharmatheutical) akipaza sauti kuwavuta abiria wengi wapande gari lake (lenye maandishi T/SEGEREA - MAKUMBUSHO VIA MANDELA ROAD kwa mbele) waachane na daladala zingine zilizo ongozana kwa mkupuo baada ya foleni kutoka M.city kuruhusiwa na kale ka traffic (ka yanki hivi huwa kana mbwembwe sana kanapoita magari pale Sayansi).

Basi bana, kachaa na begi langu mgongoni (ndani kuna laptop ya LENOVO, adapter na mouse) nikadandia kwenye seat ya nyuma kabisa shaaaaaa tuliiii na 500 yangu mkononi (mishale ya saa moja unusu hiyo giza lishatanda hapo).

"Tembeaaaaaa"
Alipaza tena sauti konda huyo baada ya abiria kujaza seat zote zilizokua wazi. Dereva kapiga gia motooo!!!

Kule back bencha niko na maduu kama wanne hivi (wako HOT kiaina) tulipanda nao pamoja pale Kituoni
Kama kawaida yangu nikiona maduu kwa daladala huwa najukuta nanywea nywiiiii (shut up my mouth ka nimetoka Sitimbi vile). Mara huyu ana Tablet, Mara huyu cjui cm gani kuuubwa full whatsapp, fb, instagram na mitandao mingine wanaijua wao. Mwanaume hata sina time nao, macho nje ya dirisha nikiwapimia boda boda wanavo risk maisha yao na abiria wao kwa kuchepuka pemben ya main road kuepuka foleni.

BASI BANA:
"Fungua nauli hiyoo!!"
Hatujafika hata ITV Konda si kaanza kudai nauli mazee!!

Mara nikackia kelele:
Jamaa: Oyaa konda bado mia hapa!!
Konda: Mia!! Kivipi???
Jamaa: Nimekupa mia tano
Konda: Eee kwahiyo.... Si chenchi nimekupa hapo??
Jamaa: Umenipa mia, bado mia
Konda: Nauli mia nne
Jamaa: Acha ufala, we si umetangaza mia tatu wewe, unadhani ungesema mia nne ningepanda mimi??
Konda: Usiniletee giza hapa, nauli iliyotangazwa na SUMATRA ni mia nne kila kituo, kama ulisikia mia tatu basi lilikua lile gari la mbele, sio mimi. Kama unaona nakudhulumu nenda kashtaki polisi!!

Duuh.. Abiria wengine wakawa wanam support jamaa:
Abiria: Lakin we konda, mbona mwenyewe ulisema nauli mia tatu, sasa hivi unageuka!!
Konda: Nimesema hivi, nauli ni mia nne, kama vp traffic wale pale shukeni mkashitaki
(Aliongea kwa jazba akiwa point kibanda cha traffic pale sayansi)

Jamaa: Konda tutatoana nishai aisee, nipe mia yangu nasema!!
Konda: Nimekwambia hivi fanya ufanyalo mia SIKUPI. Anko nauli hapo!!
(wakat huo amenifikia mimi nyuma kule. Nikaona isiwe tabu, mbele ya warembo hawa nianze kutoa povu kudai mia, uchuro huo. Nikatoa jero yangu nikarudishiwa jiti nikatulia nywiii nackilizia vagi la jamaa na Konda.

EBANA EEE:
Kufumba kufumbua Konda kapigwa kerebu moja la mgongoni, nae akageuka kajibu mapigo kwa ngumi moja ya kidevuni kwa jamaa.. Daah Chief Engineer nashuhudia mpambano wa Big Show na Batista bureee bila kiingilio.
Zimechapwa ngumi mle, warembo sasa "Mamaa jamanii, mtatuangukiaaaa!!!" Heheheheee. Nikabaki kucheka rohoni tu.

Mwisho wa cku ikabid dereva asimamishe gari wakaamuliwa pale, gari ikaingia makumbusho tukashuka wakapanda abiria wa kwenda Segerea (wakapambane na foleni ya Ubungo mataa, achana na ile ya Tabata kwenyewe).

DAAAAAAH:
Nimefika getto nimekaa nawaza hapa hivi jamaa kisa ka shilingi jiti tu anajiaibisha mbele ya mademu mle.
Na konda nae, cjui alikua amezidisha viroba!! Katangaza mwenyewe "Makumbusho mia tatuuu!!" then anachange gia angani (kama Mwenyekiti wa Chama chetu alivofanya kwenye mchakato wa Uchaguz mkuu last year).

Heheheeee kwa kweli Ijumaa ya leo nimecheka sanaaa....

#Chief Eng.
 
Back
Top Bottom