Makufuli awajibike

Mateso

JF-Expert Member
Aug 6, 2008
259
19
Ni muda mrefu tumekuwa tukimsikia Mheshimiwa Makufuli akiwataka wavuvi wanaotumia nyavu ndondogo wengine wanaita korokoro wazisalimishe au wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria. Kimsingi wavuvi hawa wamekuwa wakijipatia riziki zao za kila siku kwa nyavu hizo ndogondogo. Sasa wengi wamesalimisha nyavu zao na hawana namna ya kujipatia mkate wao wa kila siku pengine watoto wanaweza wakashindwa kwenda shule hapo baadaye. SASA kwa nini Makufuli asiwajibike kuwatafutia miokpo ya kuwanunulia nyavu halali wale wanaosalimisha nyavu zao kwa hiyari yao ili awashawishi na wengine kusalimisha zao? Nasema hivyo kwa sababu kama mtu anajua akisalimisha nyavu zake watoto watakufa njaa hatakuwa tayari kufanya hivyo. WADAU MNASEMAJE?
 
ipo sheria ya nyavu za mtando ilipitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,.
sasa yeye anaisimamia sheria hiyo ipasavyo.
sasa tuambie huyo Waziri kavunja sheria ipi.
 
Ni muda mrefu tumekuwa tukimsikia Mheshimiwa Makufuli akiwataka wavuvi wanaotumia nyavu ndondogo wengine wanaita korokoro wazisalimishe au wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria. Kimsingi wavuvi hawa wamekuwa wakijipatia riziki zao za kila siku kwa nyavu hizo ndogondogo. Sasa wengi wamesalimisha nyavu zao na hawana namna ya kujipatia mkate wao wa kila siku pengine watoto wanaweza wakashindwa kwenda shule hapo baadaye. SASA kwa nini Makufuli asiwajibike kuwatafutia miokpo ya kuwanunulia nyavu halali wale wanaosalimisha nyavu zao kwa hiyari yao ili awashawishi na wengine kusalimisha zao? Nasema hivyo kwa sababu kama mtu anajua akisalimisha nyavu zake watoto watakufa njaa hatakuwa tayari kufanya hivyo. WADAU MNASEMAJE?
Maswali..........
1. Huyo mvuvi wakati ananunua nyavu alikuwa hajui kama kuna nyavu haziruhusiwi.........???
2. Na wenye mashamba ya bangi ambao watoto wao wanaenda shule kwa bangi hizo nao tuwatafutie mkopo.......???

SIONI SABABU YA KUMWAJIBISHA KATIKA HILI.............
 
Ni muda mrefu tumekuwa tukimsikia Mheshimiwa Makufuli akiwataka wavuvi wanaotumia nyavu ndondogo wengine wanaita korokoro wazisalimishe au wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria. Kimsingi wavuvi hawa wamekuwa wakijipatia riziki zao za kila siku kwa nyavu hizo ndogondogo. Sasa wengi wamesalimisha nyavu zao na hawana namna ya kujipatia mkate wao wa kila siku pengine watoto wanaweza wakashindwa kwenda shule hapo baadaye. SASA kwa nini Makufuli asiwajibike kuwatafutia miokpo ya kuwanunulia nyavu halali wale wanaosalimisha nyavu zao kwa hiyari yao ili awashawishi na wengine kusalimisha zao? Nasema hivyo kwa sababu kama mtu anajua akisalimisha nyavu zake watoto watakufa njaa hatakuwa tayari kufanya hivyo. WADAU MNASEMAJE?

kwani hizo nyavundogo alinunua kwa mkopo?? tangu awali alipokuwa akinunua nyavu hizi tayari zilikuwa zimepigwa marufuku sasa yeye kwanini avunje sheria kwa kununua nyavu zisizotakiwa halafu eti leo apongezwe kwa kuhamasika kuacha makosa na kurejea kwenye utaratibu.. mi nadhali hao wenye nyavu ndogoi ilitakiwa kupewa adhabu badala ya tuzo ya mkopo!
 
sijakuelewa,inamaana unataka uvuvi haramu uendelee kwa kisa cha kupeleka watoto shule au? kwani hizo nyavu zinazo hitajika zina tofauti gani ya bei na hizo haramu? na tangu waanze kufanya huo uharibifu wao hawajapata mtaji wa kununua nyavu nzuri na rafiki wa mazingira?
 
unajua tunakasoro moja WaTz, tunapenda sana kuona huruma pindi SHERIA IKISIMAMIWA VYEMA.
hii ni Ishara kuwa watu wetu hawasomi sheria, hawafatilii sheria, na wala hawajishughulishi kuutafuta ukweli.
Sheria hiyo ya mtando haina hata miaka mitatu, tangu ipitishwe, lazima Magufuli asimamie sheria na katiba kama alivyoapa kuilinda na kuisimamia.
 
Anachokifanya Dr Magufuli ANASIMAMIA SHERIA, sioni kwanini mumlaumu sheria inakataza na ndo anachokipigania
 
Mateso

Makufuli ni nani? Umekuwa great tinker I presume?
anaweza kuwa amekosea herufi za jina la huyo mtu, ila kwa muktadha na maeleza yake yanakupeleka moja kwa moja kwa mtu mmoja maarufu sana anaitwa Dr JOHN POMBE MAGUFULI mbunge wa Chato na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. mkemia,na mwalimu wa zamani.
 
Unamaana ya John Pombe Magufuli ..au Makufuli..anyway kama unamaana ya Magufuli Waziri wetu wa Uvuvi nafikiri hakuna kosa analofanya katika kusimamia sheria,ni kweli kwamba baadhi ya watoto wanawezashindwa kwenda shule lakini hilo si kosa la magufuli,bali ni mzazi anayefanya shughuli haramu za uvuvi ambazo sheria imekataza,kumbuka hakuna haki bila wajibu,maana kuna watu wanafanya kazi za ujambazi,na wanawatoto wanawasomesha kwa kazi zao hizo,je na hao wakikamatwa na kufungwa tutasema Waziri wa mambo ya ndani awajibike...bosi acha Magufuli afanyekazi yake.
 
Back
Top Bottom