Makubwa yaibuka mradi wa Umeme Kinyerezi II

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,094
MAKUBWA YAIBUKA MRADI WA UMEME KINYEREZI II.
index.jpg

SIRI kubwa imefichuka juu ya mradi kubwa wa umeme wa Kinyerezi 11, ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa mradi huo unatarajiwa kuligharimu taifa zaidi ya sh. trioni 1 mpaka kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo wa kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Japan.

Mradi huo, ambao taarifa zake zimekuwa zikifanywa kwa usiri mkubwa kiasi cha kupelekea wanasiasa na wadau wengine wa maendeleo kuanza kupaza sauti na ‘kupiga kelele’ kuhofia upotevu wa fedha nyingi kwenye mradi huo kama ilivyozoeleka kwenye miradi mingine mingi ya umeme iliyowahi kuripotiwa hapa nchini ikiwemo Richmond, IPTL na Symbion,

Taarifa za uhakika zinasema kwamba tayari serikali imewekeana mkataba na kampuni ya Sumitomo Corporation ya kutoka Japan na kwamba taarifa zinasema mkataba huo utaipelekea Tanzania kulipa fedha nyingi katika mradi huo kulinganisha na miradi mingine inayoshabihiana na huo wa KinyereziII.

Mradi huo unapangwa kugharamiwa kwa uwiano wa asilimia 85 kwa 15 zinazotakiwa kuchangiwa na serikali ya Tanzania ili mradi uanze ambapo taarifa zinasema tayari serikali ya Tanzania imeshatoa sehemu yake..

Mradi wa KinyereziII , ambao unatarajia kuzalisha megawati 240, ambapo mitambo hiyo itakuwa inatumia gesi asilia kutoka Mtwara, ambapo awali watu mbalimbali walikuwa wanapinga ujenzi huo kwa kuwa unaigharimu serikali na nchi kwa ujumla kulinganisha na miradi mingine.

Taarifa ya serikali iliyotolewa na Mkuu wa Mawasiliamo wa wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud inasema kuwa tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba mkataba huo ni halali na umesainiwa kwa kufuata kanuni na taratibu zote za kibiashara tena zenye kulisaidia taifa.

‘’Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Japan ya Mkopo wa masharti nafuu wa dola za marekani milioni 292 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawat 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO ya Japan kama Mkandarasi na sio kama Mbia’’. Ilisema taarifa ya Badra

Badra alisema ‘’Mradi huu unamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 kupitia Tanesco na hakuna mwekezaji mwengine katika mradi huu’’.

Taarifa hii ya Serikali imekuja baada ya kuibuka kwa taarifa za mkanganyiko wa gharama za mradi huo ambapo zipo taarifa zinasema mradi utagharimu dola za marekani milioni 459 sawa na Shilingi Trilioni moja ya kitanzania ikijumuisha gharama za ujenzi, uendeshaji na gharama za dharula.
 
MAKUBWA YAIBUKA MRADI WA UMEME KINYEREZI II.View attachment 318125

Mradi huo uliozinduliwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete,umegharimu zaidi ya shilingi Trilioni 1.6.
Kutokana na namna ilivyoendeshwa tenda hadi kupatikana kampuni ya Sumitomo ya nchini Japan,baadhi ya wanasiasa walipiga kelele kuhusu gharama kubwa kuliko mahitaji halisi ya mradi huo.
 
Uliozinduliwa na JK ni Kinyerezi I, unaozungumziwa hapa ni Kinyerezi II
 
Kwenye umeme mie sisemi najua ndooo shidaaaaaaaaaaaaa. Hata tukilia vipi tungo ni nyingi watatutuliza tu na hadthi zileeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Nafungu mdomo
 
Back
Top Bottom