Maktaba iliyojengwa na China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania yafungua milango kwa wanafunzi

Maktaba iliyojengwa na China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania yafungua milango kwa wanafunzi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
W020240424475314057128.png


Ushirikiano kati ya China nan chi za Afrika umegusa maeneo mengi ikiwemo sekta ya elimu. Kupitia ushirikiano huo, China imejenga, kukarabati, ama kutoa msaada wa aina mbalimbali katika shule nyingi za barani Afrika. Msaada huu wa China sio tu kwa shule za msingi na sekondari, bali pia kwa vyuo vikuu mbalimbali.

Mfano halisi wa ushirikiano huu ni Taasisi za Confucius ambazo zimeanzishwa katika vyuo vikuu vya nchi nyingi za Afrika, ikiwemo Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) cha nchini Tanzania. Kupitia Taasisi hizi, vijana wengi wamefanikiwa kubadili maisha yao kutokana na mafunzo ya lugha ya Kichina, yaliyowawezesha kupata ajira katika kampuni nyingi za China barani Afrika.

Kwa upande wa UDSM, ambacho ni Chuo Kikuu kikubwa zaidi nchini Tanzania, kuna maktaba mpya ambayo imejengwa na China, na imekuwa msaada mkubwa kwa walimu na wanafunzi katika kuboresha mafunzo na utafiti. Maktaba hiyo iliyofunguliwa mwaka 2018 kwa kuungwa mkono na serikali ya China, imeendelea kuwa moja ya vituo vikubwa na vya kisasa zaidi vya mafunzo katika kanda ya Afrika Mashariki, na sasa, maktaba hiyo inatumika sio tu kama kituo cha mafunzo, bali pia kama kichocheo cha uratibu wa kimataifa.

Ikiwa na uwezao wa kuhudumia watumiaji 2,500 kwa wakati mmoja, maktaba hiyo yenye mtandao wa kasi ya juu, upatikanaji wa kidijitali wa majarida ya kimataifa, na maabara ya kisasa ya compyuta, kwa wanafunzi wengi imekuwa sio sehemu ya kujisomea tu, bali pia mazingira rafiki kwa ajili ya utafiti na ukuaji wa kitaaluma.

Stanley Kulanga ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu, anasema maktaba hiyo imekuwa na umuhimu mkubwa sana katika maendeleo yake ya kitaaluma. Anasema tangu alipoanza masomo yake ya shahada ya uzamivu, maktaba hiyo imekuwa sehemu nzuri kwake kujikita zaidi katika masomo na kupata nyaraka anazohitaji, na ameongeza kuwa, mara nyingi anakuwa wa kwanza kuingia na wa mwisho kutoka kwenye maktaba hiyo.

Kwa upande wa wahadhiri na watafiti, maktaba hiyo imekuwa na umuhimu mkubwa sana kwao. Mhadhiri mwandamizi katika Idara ya Teknolojia ya Ufugaji Samaki katika Kitivo cha Teknolojia ya Sayansi ya Ufugaji na Samaki, Samwel Mchele Limbu, anasema idadi kubwa ya rasilimali za vitabu vya kidijitali na vilivyochapishwa imekuwa muhimu sana katika kuendeleza kazi yake. Anasema anatumia maktaba hiyo kuandika nyaraka zake, na hivyo kumfanya kuwa mtafiti bora zaidi wa mwaka kwa miaka miwili mfululizo. Mtafiti huyo anaielezea maktaba hiyo kama ushuhuda wa ushirikiano kati ya China na Tanzania, akisema inatimiza mahitaji ya kubadilishana uzoefu kwa vizazi, jambo linaloendana na dira ya Tanzania ya maendeleo jumuishi yanayoongozwa na elimu bora.

Maktaba hiyo si kwamba inatumiwa na wanafunzi na wahadhiri wa Tanzania pekee. Kwa mujibu wa Kelefa Mwantimwa, mkurugenzi wa huduma za maktaba katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi kutoka China, Malawi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara nying wanaitumia maktaba hiyo, pamoja na wasomi kutoka Marekani, Ujerumani na Uingereza. Anasema awali, maktaba hiyo ilikuwa inajaa sana watu kwa kuwa ilikuwa ndogo, lakini sasa, wanajivunia kuwa na maktaba kubwa nay a kisasa zaidi inayosaidia ufundishaji, kujifunza, utafiti, na uvumbuzi.

Licha ya masuala ya kitaaluma, maktaba hiyo imekuwa sehemu inayopendelewa kwa ajili ya mikutano ya kimataifa, semina, na makongamano. Mashirika kama Umoja wa Mataifa na mashirika yake mara nyingi yanatumia maktaba yao katika shughuli zao, huku mawaziri wa Tanzania na taasisi za kikanda wakitumia sehemu hiyo kwa mafunzo na majadiliano.

Mwantimwa anasema, kwa wanafunzi kama Kulangwa, maktaba hiyo inasimama kama alama ya fursa na uhusiano unaokua kati ya Tanzania na China. Pia anasema, maktaba hiyo inaakisi uhusiano wa kina, na idadi kubwa ya Watanzania wanapata fursa ya kuendelea na masomo yao ya juu nchini China kupitia ufadhili wa serikali ya China.
 
Back
Top Bottom