Makosa aliyofanya Membe yanaongeleka lakini sio Sitta

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,051
Habari wakuu,

Siku za hivi karibuni mh. Membe amekuwa akiikosoa Serikali ya Magufuli, kitendo hiki kimeanza kumjengea maadui ndani ya chama hicho kiasi kwamba kumekuwa na matamko ya jumuia mbalimbali za chama hicho na wanachama wengine wa chama hicho, Membe angeishia hapohapo tu angeonekana anatumia demokrasia yake ya kukikosoa chama chake, lakini akanukuliwa akitoa kashfa kwa ukawa hapa ndipo alipofanya kosa ambalo atakuja kulijutia hapo baadaye.

Lakini pamoja na makosa haya ya Membe bado nikiri kuwa ni makosa yanayosameheka kama ataomba msamaha kwa upande wowote iwe ukawa au ccm. Mtu ambaye hata akiomba samahani kwa upande wowote iwe ccm au ukawa hawezi kupokelewa ni Sitta huyu alikuwa ni msaliti kwa pande zote za vyama vya siasa yaani, chama tawala na vya upinzani, lakini wananchi hawatamsahau kwa kuwaharibia nafasi nzuri ya kupata katiba mpya kwa njia ya amani bila kumwaga damu, kitendo chake hicho kilipelekea hasara kubwa sana ya fedha ya walipa kodi wa Tanzania.
 
Yaani unakuta jamaa linakorofishana na majirani wote. Sasa sijui ikitokea dharula nani atamsaidia!
 
Lakini nanyi wanaukawa niwanafiki si mlisema ni haki Yake kikatiba kutoa maoni na mkaenda mbali zaidi kwakumwita shujaa sasa mnaposema katoa kashifa kwa ukawa eti hapo ndo kafanya kosa, kosa lipi hapo?
 
Lakini nanyi wanaukawa niwanafiki si mlisema ni haki Yake kikatiba kutoa maoni na mkaenda mbali zaidi kwakumwita shujaa sasa mnaposema katoa kashifa kwa ukawa eti hapo ndo kafanya kosa, kosa lipi hapo?
Mkuu membe anataka kujionyesha kuwa yeye ni wa vuguvugu, hayupo kwenye baridi wala moto, jambo hili Mungu alilikataza
 
Sisi ukawa tupo tayari kukosolewa tatizo sisi alitukashifu sio kukosoa kama alivyofanya kwa ccm
 
Membe yuko sahihi kwa maoni yake...he is a free man

Sitta yule ni fwaaala ameigharimu sana nchi hii
 
Nimakosa ya kipuuzi kumshikilia ndugu six kuwa ndiye aliyeharibu Katiba. Nilini watu wataelewa kuwa alichokifanya nikile alichoagizwa na chama. It Is a collective misbehaving na wahusika ni wabunge Wa Ccm na waliokubaliana nao.
mfano Lowassa alikosea tukasema shida ni system na watu wakaelewa,mbona hili tunashindwa kulielewa wakati nalo linatokana na system? Tunabaki mng'ang'ania mtu mmoja tuu...
ukifundishwa mayai mawili ongeza mayai matatu jumla mayai matano huhitaji Tena kufundishwa maembe mawili ongeza matatu jumla mangapi... la unakaubongo kagonjwa!
 
Back
Top Bottom