Milango miwili na hata mitatu kwa mabasi ya abiria yana matumizi yake... Mlango wa mbele ni wa kupandia na mlango wa nyuma ni wa kushukia.. Hivyo neno "nyuma" bado litakuwa linatumika
Kwenye Ikarus, mabasi ya zamani ya UDA yalikuwa na milango mitatu, haya yalikuwa ni marefu zaidi, na walikuwa na yale ya milango miwili... Ila kwa wakati ule idadi ya mabasi ilikuwa ndogo ukilinganisha na idadi ya abiria. Hii ilisababisha kuweko na makonda wawili, moja mlango wa mbele na moja mlango wa nyuma... (kwa ikarus mlango wa kati haukuwa na konda)
Anyway hiyo ilikuwa ni 70's! Sidhani kama utaratibu huu utarudiwa tena, hii ina maana dereva pamoja na kuendesha basi ndie atakuwa konda! Maana yake mlango wa kati na wa nyuma utatumika kwa kushushia abiria..