Makonda usipoteze muda wako

Hoja yako ya wanandoa kuchepuka ukafungwa miaka thelasini ni mfu na ndoto

Wewe na bashite ni mazumbukuku, badala mboreshe huduma za kijamii mnahangaika na vikojoleo na mioyo isiyowahusu
 
Hoja yako ya wanandoa kuchepuka ukafungwa miaka thelasini ni mfu na ndoto

Wewe na bashite ni mazumbukuku, badala mboreshe huduma za kijamii mnahangaika na vikojoleo na mioyo isiyowahusu
😂😂 vikojoleo ndo nyapu au!
 
👆 hiyo umetoa maoni fake kabisa..!!
 
Makonda yupo sahihi kabisa muacheni afanye hiyo kazi kwanza kabisa ujue amesema atashirikisha wajumbe wa nchi zingine kuona kwamba wao wanafanyaje kushughulikia mambo kama hayo. Ukweli ni kwamba tanzania yetu bado ipo huru sana kufanya mambo ya kijinga hakuna mwanamke anayependa kutapeliwa pili ujue unamnyanyasa mtoto kwanini umpe mtu mimba halafu umtelekeze na mtoto kwanini usimchukue basi mtoto wako kama unaweza ukamtunze wewe? hebu angalia kama marekani ukizaa na mtu lazima utunze mtoto na usipofanya hivyo pesa zako zote zinakatwa na serikali then inaenda kwa mtoto. sasa tanzania yetu lazima serikali ianzishe utaratibu kama huo hasa kwa wale walioajiriwa serikalini na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO'S) . Kwa wale ambao hawakuajiriwa wamejiajiri basi serikali iangalie sheria yake mpya ya kuwabana hao.
1.kwa kufanya hivyo ongezeko la watoto mitaani litapungua.
2 Ndoa zitaheshimiwa na idadi ya ndoa zinazovunjika kila kukicha zitapungua kwani ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya michepuko na watoto wa nje kuongezeka.
wanaume watakuwa waaminifu na pia watakuwa waoga wa kuchepuka kwa kuhofia mimba za nje.
3. Ugomvi wa mali baina ya watoto wa nje na wa ndani ya ndoa utakwisha kwa kupitia sheria hiyo mpya.
4.Ukimwi utaisha kama sio utapungua kwani michepuko imekuwa mingi hadi kuwaambukiza maradhi hata wasiokuwa na hatia
5. Kanisa litakuwa limepata msaada mkubwa kwani ndoa zitadumu hivyo wachungaji nao watapumzika kwa kusuluhisha migogoro ya ndoa kila siku.
6 Ukimpa mtu mimba hata kama usipomuoa lakini lazima utatunza hivyo mtoto hatateseka

Mwisho kabisa nakuomba Muheshimiwa makonda zingatia hili ukifanikiwa tu nitakutafuta nikupe zawadi yako manake hata mimi nimechoshwa kabisa na hizi tabia za watu wasiokuwa waaminifu usiogope wanaokubeza kwani watanzania wengi tumesahau majukumu yetu tumehamia wote kwenye michepuko kama vile ndio kazi iliyobaki. inawezekana maombi ya wanandoa yanakwenda kujibiwa sasa kwa kupitia wewe. Mungu akutangulie ufanikishe hili Makonda wangu
 
kwanza atazuiaje suala la Nyumba ndogo? Pili anajuaje kuwa wadanganyifu wa ndoa ni wanaume pekee? Tatu ni kwa namna gani hiyo database ya ndoa itawaondolea wachumba watarajiwa kutapeliwa? Maana mtu anaweza asiwemo kwenye hiyo kanzi data lakini bado akamliza mchumba wake!
 
Duhhh...Taikon waFasihi hapo aisee......duhh sijawahi kuhisi wewe ni mnoko kiasi hiki....unataka hii nchi iwe kama tupo peponi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Umeongea vizuri sana ila ushauri wako.....samahani... kwangu mimi nauona wakidikteta sana.


Kuhusu bikira kwa mwanamke inaweza kutoka ata kwa michezo ya kawaida tu na sio kwa zinaa, na sijui kama itasaidia kwa kusema tu...mimi sijawahi kufanya mapenzi, ukaridhika kuwa yupo bikira..na kama utaruhusu utetezi huo basi wale ambao hawana wote wataegemea huko.

Sifikirii pia kama mwanamke atasema hajawahi kufanya mapenzi lakini bikira haipo serikali ianze kupima kama hiyo sehemu ya uke imewahi kupitiwa na mzigo flani hivi....tukifika huko itakuwa ni udhalilishaji......

Mi nasema hivi hiyo kanzu data iwepo kwa wote kama leo hii tunaweza kumuona wakili aliyeruhusiwa kufanya kazi hiyo ndani ya sekunde tu...itakuwa vizuri pia kwa wanandoa ukitaka kujua "Muda wa Ukombozi" kaoa na kamuoa nani majina yatokee na picha zetu namaanisha mimi na mke wangu, halikadhalika iwe hivyo na kwa wanawake pia tukiwapekua tuone hadhi zao pia.

Halafu wakati mwingine mapenzi ni neno ukilinyambua vizuri utakuta kuna upendo ndani yake, na nguvu yake ni kubwa, ukitaka kuleta ubaguzi hapa, mwanamke ukimuhitaji kidogo mara andika barua, mara fuata taratibu wanawake wengi watabaki manungaembe.

Mi naona utaratibu huu uendelee ila mh. Makonda achukue ushauri wangu hapo, hii itatusaidia sisi wanaume, kama ni muislamu kuna ruhusa ya kuoa wake wanne, kwahiyo mwanamke atajua anapambana yeye atakuwa wangapi, kama ni mkiristo na utaratibu wa dini ni kuwa na mwanamke mmoja ni kuangalia jinsi gani unaweza kuongeza kimila.......

Mila zetu za Kitanzania ata afrika sijawahi ona kuna ukomo wa kuoa kwahiyo kama umeoa na bado umependa mwingine tena, hakuna namna unaoa kimila maisha yataendelea.

Ahsante sana...nimefurahishwa na huu uzi..uangu ni hayo machache.
 
sasa ndio umeandika nini...? ebu muacheni makonda afanye kazi kwenye mkoa wake...
 
Hongera kwa mawazo yako Chanya.....
Napenda na kuvutiwa na utangulizi ulioanza ila ukaja kuharibu kwenye Namba.

Kuanzia 1 mpaka ya mwisho hakuna uhalisia...mfano mdogo tu kwamba pamoja na sheria kalo ya ubakaji yenye adhabu kali lakini Bado watu wanabaka, na wengine pengine hawafungwi, aidha kwa sababu mbalimbali.

Umtajaye hatoweza kubalidi sheria wala yeye hahusiki moja kwa moja katika kuzitunga wala kuanzisha muswada wa sheria.

Hiyo namba 1 tu inakufanya ujikute umewatengenezea watu biashara ya kupata pesa SABABU WATAANZA KUUZA UNGA WA DAWA ZA KURUDISHA BIKRA tena kwa kunadi kama zinavonadiwa za NGUVU ZA kiume mara vumbi la kongo, mundende, super nini sijui.....n.k

Nyumba za kulala wageni sio ndio UWANJA WA MKP pekee ambapo mechi za uzinzi zinachezwa ila maeneo ni mengi na madanguro na vyumba vya short time vya wamiliki halali kabisa wanaouza vinafahamika na vingine ni siri kubwa labda ukiwa mteja.

Hitimisho.
Hoja yako ya msingi binafsi na wanavuoni wengine na wasio wanavuoni watakuwa wamekuelewa "KUWA WANAWAKE WAO WENYEWE NDIO WANAOCHUKUA NAFASI KUBWA KATIKA KUFANYA WATAPELIWE"

Naomba ibaki hivo Sababu kama mwanamke ataweka KUOLEWA KAMA NI FIRST DEMAND BASI MWANAUME ATAKUWA HANA BUDI....

Naomba kuchangia na kuwasilisha
Asanteni
 
Kwani Baba Keagan kaja na mpya ipi?

Maana jamaa huwa anaweza toa matamko hata kumi ndani ya mwezi...
 
Huezi kuwalazimisha watu kuishi pamoja,mnaona kwa kuwa watanzania ni hewala hewala kila mnalosema sasa mnataka kutuingilia hadi vyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…