Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Christian Makonda, ameendelea na ziara zake za kampeni ndani ya jimbo hilo, ambapo leo Oktoba 18, 2025, amekutana na wafanyakazi wa saluni wanaojihusisha na kazi ya ususi na urembo.
Katika mkutano wake na wafanyakazi hao, Makonda amewahamasisha kuhimiza wateja wao pamoja na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Amewaomba kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi wa CCM akiwemo Mgombea Urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yeye kama Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini, pamoja na Madiwani wa CCM.