Makonda: Simwogopi Magufuli

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
makonda1-620x308.jpg

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amedai kwamba hafanyi kazi kwa kumwogopi Rais John Magufuli, anaandika Regina Mkonde.

“Nafanya kazi zangu ipasavyo na si kwa woga wa rais. Namuomba Mungu anisaidie nisitumie cheo na madaraka yangu kugandamiza wengine,” amesema Makonda.

Hata hivyo, Makonda amejidhihirisha kuwa kiongozi mbabe. Mwaka juzi alimvamia Jaji Joseph Warioba, katika mdahalo wa katiba Mpya, jijini Dar es Salaam, akamrushia makonde na m

dahalo ukavunjika.

Baada ya hapo aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni. Desemba mwaka jana, alitumia mamlaka yake vibaya kwa kuamuru polisi wamkamate Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, baada ya wawili hao kutofautiana kauli wakiwa kwenye usuluhishi wa mgogo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Tooku na menejimenti, jijini Dar es Salaam.

Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhiwa ofisi na Said Mecky Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sadick amehamishiwa mkoani Kilimanjaro kushika wadhifa huo.

Kwenye makabidhiano hayo Makonda amevitaka vyama vya upinzani kuachana na siasa za ubaguzi na kwamba, wanapaswa kufanya siasa wakati uchaguzi utapokaribia.

“Huu si wakati wa kuendekeza siasa za kibaguzi, si wakati wa propaganda za kuchafuana, tufanye kazi. Wananchi wanahitaji kuona mabadiliko kama mlivyokuwa mnajinadi kwenye kampeni za uchaguzi, subiri mwanzoni mwa waka 2020 ndiyo muanze siasa.

“Nitafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, katiba na ilani ya CCM katika kutatua changamoto za Jiji la Dar es Salaam,” amesema Makonda.

Akikabidhi ofisi hiyo, Sadick alimwambia Makonda kwamba jiji hilo haliongozwi na upinzani kama ambavyo inaelezwa na vyama hivyo.

“Dar es Salaam haijakamatwa na upinzani, bali ni mameya na wabunge ndiyo wengi. Hii haimaanisha kwamba jiji linashikwa na upinzani,” amesema Sadick.

Kwenye makabidhiano hayo Sadick amesema, atakapokwenda kuanza kazi Mkoa wa Kilimanjaro hatapambana na vyama vya siasa bali atashughulikia maendeleo.

“Siendi kupambana na vyama vya siasa mkoani Kilimanjaro, ninakwenda kusimamia maendeleo, awe kiongozi wa CCM au Chadema sawa, sote tuna nia ya kujenga nyumba moja,”

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Kijana yule mzee hatabiriki. Kuwa makini na ukisemacho. Shauriyooo.
 
Rais aliwaagiza mkawatumikie wananchi muachane na siasa sasa naona mmeanza siasa. Kuwa mwana Ccm inahitaji kwanza kunitoa ufahamu kama hawa wakuu wawili wa mikoa.
 
Upinzani hongereni sana kwa kushika jiji ambalo ndo kitovu cha uchumi wa tanzania.
 
Mimi nimeishia apo kwenye neno CCM huwa nikiliona hili neno nakosa raha kabisa,moyo unauma kweli. Hiki chama kimeutibua sana mtima wangu.
 
Kama yeye makaonda anafanya kazi kwa kuzingatia kanuni,katiba na ilani ya ccm,ivyo tutarajie weledi gani kaz ktk kazi zake?kama sio ufisiemu?!
 
Mwandishi na mtoa mada ameamua kukuza hilo neon, KIUFUPI LABDA Atafanya kazi kwasabab ni wajibu wake na sio kila atakachofanya kwa hofu ya kufukuzwa kazi, ina maana ataifanya kazi kwa moyo mmoja, Na sio kwa woga woga wakumridhisha au kujionyesha kwa Rais n.k.
 
Waziri au mbunge kwanza? Huwa napata shida kidogo, RC na Ubunge upi una deal? Maana naona RC wanakimbilia sana ubunge! Au ndio zile za ujumbe wa board? Ambazo zimepigwa chini? Au kukimbia majukumu na lawama za RC? Napenda kujua!
 
Back
Top Bottom