Makonda, onesha Vyeti vyako halali wanaokutuhumu waaibike

Yani huyu Mako anawalaza macho Sana. Halafu watu wamechukua uongo wa bipolar Mange na kugeuza mada Yule ana stress za talaka kila mwenye mafanikio ni adui yake. Poleni Sana awadhibitishie nyie nani?? Subiri aliyemuajiri aombe adhibitishe tofauti na hapo endeleeni tu kupiga makelele.
Ndugu lisemwalo lipo kama halipo laja
Labda km ulisoma na Paul makonda na ukamjua kwa jina hilo toka primary to chuo km hukusoma nae ni bora ukae kimya tuu.
Huu mchezo hauhitaji hasira,tuendelee kuangalia utaisha vipi.
 
Kwa niwatake nyie wote mnao potosha watu kuwa dar ni kubwa kuliko mikoa yote Tanzania mfute kauli hizi Na mtupe ushahindi wa km squares za mji huo kwa upana Na urefu ukilinganisha Na Mimi mingine Pili suala la makonda kutumia akili au vyeti vya mtu mwingine siyo shida nikipaji pia suala lilipo ni watuhumiwa wasitafute njia za kijinga za kujitetea Jana pia nimesoma sehemu kuna mama anadai mtoto wake alitongozwa Na makonda alipokataa akapewa tuhuma za madawa ya kulevya hivi kweli unaingia akili hata kidogo
 
Awe Bashite asiwe Makonda, hakuna haja ya kumueleza chochote mtu yeyote, ameteuliwa na Rais kama yeye kwa umbo na sura yake na utendaji wake. Awe na elimu asiwe na elimu. Hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji uteuzi wa Rais, katiba inatuelekeza hivyo. Kama akiulizwa na rais sawa, lakini sio mchezea pembeni yeyote yule, huo ndio utawala wa sheria!
Km watanzania tunawaza na kuona mambo kwa mitazamo hii naona Tanzania ya viwanda ipo km mbingu na nchi vile
Kwani hao wote waliotumbuliwa na Rais waliteuliwa na nani?
Tanzania's we have a looooong way to go!!!!!
 
Msema chochote humaliza maneno yote kamwe habakizi maneno ya akiba kwa sherehe ijayo.
Ukimya una jambo, ndio busara, mda ukifika msema chochote atanywea.
 
Kuna Mwl wangu mmoja aliwahi nambia "usiyaogope majibwa yanayobweka sana!" Kwa ule utoto sikuweza kumuelewa!
 
Hatakaa iwe rahisi namna hiyo mi ni bingwa wa kukaa mbele ya media lakini c kwa hili mkuu
 
Ana

Hana

Faizafoxy yu mapumziko leo.
Hapa ndio matumizi yasiyo sahihi ya herufi h yanapobadili maana ya neno kabisa. Kutoka hana tabia nzuri hadi ana tabia nzuri. Huu ugonjwa sijui umetokea wapi na umeathiri vijana wetu kabisa. Inawezekana na walimu kadha nao ni waathirika. Sasa ongea naniliu (sijui ina maana gani ) na kadhalika.
 
Kwako Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,

Hongera na pole kwa jukumu ulilopewa la kuongoza jiji kubwa kuliko yote Tanzania. Ni imani yangu unalimudu jiji vizuri kabisa hata kuiridhisha mamlaka yako ya uteuzi na kufikia hatua ya kukupongeza hadharani tofauti na wateule wengine.

Napenda kukupongeza tena kwa ujasiri uliouonyesha wa kupambana na madawa ya kulevya kitu ambacho wengi waliopita katika nafasi yako hawakuwahi hata kujaribu japo kwa kunong'oneza tu, kwa hilo nakupongeza hadi hapo ulipofikia ingawa kuna makosa uliyoyafanya ila naamini ni ujana tu na ndio wanasemaga 'ujana maji ya moto'

Mheshimiwa mkuu wa mkoa,baada ya kukupongeza sasa niende moja kwa moja katika kile kilichonishawishi kuandika waraka huu kwani sikuandika ili kukupongeza tu,kuna jambo..

Mheshimiwa mkuu wa mkoa,ni siku kadhaa sasa tangu uanze kutuhumiwa mitandaoni eti wewe umeiba/umenunua jina la mtu aliyesoma kwa bidii na kufanikiwa kupasua vyema kunako darasa na umetumia cheti chake kujiendeleza kimasomo,kwani wewe cheti chako kimedhoofu sana na hakikuweza kukubeba ufike kule unakotaka kufika.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa,wengine wamefika mbali kabisa na kuonesha kukujua kupitiliza na kudai eti wewe sio Paul Makonda eti Paul Makonda ni huyo wanaedai wewe unatumia cheti chake, eti wamekutaja kwa jina la Daudi Bashite wakidai ndio jina lako halali.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, tuhuma hizi zinazoelekezwa kwako zimeshika kasi kuliko moto wa kifuu pale kinapokolea na hazikomi siku hadi siku na sioni zikikoma bila kuwepo wa kukanusha.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, wewe kama kiongozi ni jambo la busara sana kujitokeza ukiwa na vyeti vyako vyote pamoja na cheti chako cha kuzaliwa ili kuwaziba midomo wale wote wanaodai ulitumia jina lisilo lako kujiendeleza kielimu..sio busara wewe kuendelea kudai hizo ni tuhuma za mtandaoni eti tuziache mitandaoni,ni kwanini tuziache mtandaoni zikiendelea kukuchafua wakati upo hai na unaweza kuita vyombo vya habari vikafika na ukamwaga ushahidi wote wa kuwaziba mdomo wale wanaokutuhumu kila siku?

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, pia ni vizuri ukamtafuta huyo bwana wanaedai unatumia jina lake ili uwadhihirishie mbele ya wanahabari kwamba ni mfanano wa majina tu!

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, sioni kama ni vizuri kila unapotuhumiwa ujifiche katika mwavuli wa madawa ya kulevya, eti kwamba kila wanaokutuhumu ni wale uliowaumiza katika vita yako ya kupambana na madawa ya kulevya, hapana tuhuma nyingine ni rahisi sana kuzimaliza na sio kutumia vita dhidi ya madawa ya kulevya kutafuta huruma ya wananchi.

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, kamwe usiwasikilize wale wanaokudanganya eti kukutaka uendelee kunyamazia tuhuma kama hizi za kutumia cheti cha mtu kujiendeleza. Hao kaa ukijua kabisa hawakutakii mema, wanakuharibia! Kila inapokuja tuhuma dhidi yako wanakukingia kifua kwa kudai hao wanaokutuhumu ni miongoni mwa walioumizwa na vita yako dhidi ya madawa.. Tuhuma kama hizi ni vizuri sana kutokujificha chini ya mwavuli wa madawa ya kulevya na ukajitokeza kizijibu kwa ushahidi ili kuwanyamazisha hao ambao unaamini wanakutuhumu kwa kuwa uliwaumiza kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya.


Mbali na hapo mheshimiwa mkuu wa mkoa nategemea utapitia waraka huu, na kama utaelewa basi utafanya vyema kuzimaliza kabisa tuhuma zinazoelekezwa kwako, kwani tuhuma hizo sio ndogo na pia sio nzuri kwa kiongozi.

Jipange, jitokeze, uyamalize!
Kwa namna ninavyomjua Daudi kwa kashfa kama hii angekuwa na Cheti angekitoa mbele ya hadhara lakini ndiyo hivyo keshanasa tunduni pale alipo anatamani arudi chekechea
 
Mtumishi wa Mungu anasimama Madhabahuni nakuamiisha Umma kuwa anavyeti Feki vya Paul Makonda kikiwemo kile anachodai Makonda Alipata Zero.

Maswali yakujiuliza
1. Gwajima ametoa wapi cheti chenye Zero kwakua serikali huwa haitoe vyeti kwa watu wenye zero?

2. Kama kweli Makonda anatumia majina mawili tena mbona Gwajima hatuletei hati ya Mwanasheria ya Makonda kubadili jina?
3. Je nilini Baraza la mitiani limeanza kutoa vyeti kwa mtu yeyote aliehitaji hatakama sio vyake?

4. Je inawezekana vipi Makonda na Gwajima wote kumiliki vyeti original vya mtu mmoja??

"watu wangu wanaangamia kwakukosa Maarifa "
Tulia dawa ikuingie taratibu utapona wewe na buku 7 wenzio wa Lumumba mmezoea kughushi nyaraka za serikali na hata yule Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa sasa alishawahi kughushi Umri wake sasa ifike mahali tuseme huu mchezo basi kwa kuanza na Daudi Bashite mwambieni aweke cheti hizo kelele hazisaidii kufunga hoja hii
 
Kuna viongozi wakubwa serikalini wenye elimu kubwa na vyeti vizuri lakini linapokuja suala la utendaji kazi ni sifuri, uwajibikaji ni mbovu, hata kama ikibainika ni kweli makonda alitumia vyeti feki bado wananchi tunamuhitaji sana especially kwenye kipindi kama hiki,makonda amefanya mambo makubwa na magumu ambayo viongozi hao mnaosema wasomi wa vyeti original hawakuvifanya, makonda ni kijana jasiri na mwenye uthubutu,Tanzania tunahitaji kiongozi kama makonda, Mungu ana makusudi kutuletea makonda,nyie endeleeni kupiga makelele but still makonda ataendelea kuwa makonda.


Na gwajima kama unadai una vyeti vya makonda kabla haujavitoa hadharani tunakuomba mtumishi wa Mungu utuonyeshee vyeti vyako na wewe ulivyosomea uchungaji,hapo utakua umefuta mzizi wa fitina.
Usipindishe mambo-Bashite anakabiliwa na kosa la jinai, na kwa watu makini wakati wewe ukiandika huu uzi alitakiwa awe mahabusu akiandika maelezo tayari kufikishwa kortini?
 
Uchungaji nini? Ulizia kule marekani kama wachungaji wanajipachika tu kama huku mtu akilala akiamka mchungaji, wamejaa utapeli, wizi na umalaya

Before commenting about makonda, tuonyesheni kwanza hivyo vyeti feki acheni kupiga makelele kama wanawake wa kimakonde, shukrani, no evidence no right to speak
Ufeki wa Makonda wala hauhitaji kusubiri uonyeshwe vyeti, if you are serious, kazi zake zenyewe zinathibitisha ufeki wake! Na kwa hulka yake tuhuma hizi zingekuwa za uongo Mawingu FM wangekuwa wameishampa airtime ya kufa mtu na vyeti angeenda navyo studio kukanusha!
 
Hivi kama ni kweli Bashite alichukua cheti cha mtu (ni kosa), lakini waajiri wake(walioshika mpini) wanamhitaji, hawawezi kutoa order kwa NECTA kutengeneza cheti chake kupoteza ushahidi? Najaribu kufikiri tu!
umefikiria sana
 
Back
Top Bottom