Makonda, kwanini machinga na sio mateja/vibaka?

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,624
3,652
Hatimaye machinga waliokuwa maeneo ya Ubungo kuelekea barabara ya Mwenge wameondolewa jambo ambalo sipingani nalo.Kinachonipa utata nikuwaona mateja wakitamalaki Ubungo darajani na iliyokua stendi ya magari ya Tegeta maeneo ya Ubungo.

Pia ukitembea nyuma ya ukuta wa TANESCO kama unaenda uwanja wa riverside kuna mateja wanatishia wapita njia,wanavuta bangi hadharani sijui niili iweje,na mbaya zaidi wanachangisha hela kwa kila anaepita pale eti ulipie kivuko.Jamani nchi hii haiishi maajabu.

Makonda na Ally Happi ondoeni hawa wala unga watakuja kuua watu pale mtoni na mateja wa Ubungo darajani polisi wamewashindwa sijui maana wanatambaa tu mjini kwa kunyanyang'anya watu simu utadhani ni zao.
 
polisi wapite hata sasa mateja hayo yanavuta bangi na yanatafuna chapati hapa riverside pembezoni mwa tanesco
 
Mateja si ndiyo wanaowauzia madawa??Sasa mnadhani wakiwatoa watapata wapi Wateja wa madawa yao??Maana Professor aliyebaka Mwanafunzi alisema ma Bungeni watoto wao ndiyo madrug lord
 
Ally Happi acheni kufukuza wanaobangaizatu na kuwaacha hawa mateja wanatesa watu mjini hapa kama RPC kashindwa kazi aombe mapumziko
 
Back
Top Bottom