TangataUnyakeWasu
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 1,268
- 1,587
Nimeinakili kutoka KWA Newton Chamkongo
Waandishi wa DAUDI ALBERT BASHITE
Kwenda Ziarani Koromije:
Kiongozi wa Mkoa anayesemekana kutumia jina lisilo lake ameandaa ziara ya Waandishi 10 watakaondoka kesho kuelekea Mkoani Mwanza. Waandishi hawa watakuwa na kazi maalumu Jijini Mwanza, katika Sekondari ya Pamba na Kijijini Koromije.
Kulingana na hadidu za rejea za ziara hii, waandishi watakutanishwa na kuongea na ndugu pamoja na walezi wa Kiongozi wa Mkoa na watatembelea Sekondari ya Pamba—Mwanza. Katika Sekondari hii watapata wasaha wa kupewa taarifa mbalimbali kuhusu Kiongozi wa Mkoa na kuongea na uongozi wa Sekondari.
Baadaye waandishi wataelekea Kijijini Koromije ambako watatakiwa kuwahoji watu kulingana na orodha iliyotolewa na Kiongozi wa Mkoa.
Kazi itakamilika kwa kuandaa taarifa katika mifumo mbalimbali ya kieletroniki (maandishi, sauti na video) zitakazolenga kuonyesha kuwa yote yaliyosemwa na kushuhudiwa juu ya Kiongozi wa Mkoa ni uongo. Taarifa kamili kutoka katika ziara hii zitarushwa mitandaoni na kupelekwa kwenye vyombo vya habari.
Lengo la ziara hii si kuibua ukweli bali kutaka kuufanya ukweli uchanganyikiwe kama njia ya kufifisha sakata la “BASHITE” Ifahamike kwamba huu ni muendelezo wa mikakati ya Mwana Kipenzi cha Mfalme baada ya kufurahia keki ya mwaka mmoja madarakani. Nakuuliza; hivi mawaziri waliambiwa wakibainika kufanya sherehe baada ya kuteuliwa watafanywa nini?