Makonda atakuwepo leo, kesho na Ikiwezekana hata milele

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,112
Kwa kwa muda wa wiki kadhaa sasa jina la Makonda na Bashite limekuwa gumzo kila kona ya nchi na nje ya mipaka ya nchi.

Kwa madudu yaliyoanikwa na vituko vya RC huyu wengi tulitegemea leo asingekuwepo madarakani ila nawahakikishieni atakuwepo leo, kesho na hata milele ikiwa tu Raisi Magufuli atakuwa bado raisi wa nchi hii.

Makonda hakuanza haya juzi au jana kijana anajua kutumika. Alituhumiwa kumchapa kibao Mzee Warioba. Pia alikuja hadharani kumpinga Lowassa na akatoa ahadi ya kijasiri na watu wakauliza hili huyu kijana ujasiri huu anautoa wapi?

Matukio na mambo yote anayofanya Makonda yamepata baraka zote na kuratibiwa vyema kutoka ofisi kuu ya nchi hii. R. Mengi jana aliuliza kibuli hiki huyu kijana anakipata wapi? Jibu ni simple kiburi anakipata kutoka kwa mkuu wa nchi.

Makonda ni M/kiti wa kamati ya Usalama wa Mkoa lakini hana mamlaka ya kuamrisha wale Polisi wanaovaa makirikiri. Wenye mavazi ya makirikiri si Polisi wa Kawaida wala si JWTZ wale ni special unit na mwenye mamlaka nao ni Mkuu wa nchi. Sasa iweje Makonda atembee nao??

Nape jana kaunda tume lakini tunatakiwa tujue kwamba lolote litakavyokuwa Nape hana mamlaka ya kumwajibisha mkuu wa mkoa sababu si yeye aliyemteuwa. Hiyo ripoti itakwenda kumshitaki Makonda kwa mkuu wa nchi ambaye ni yeye aliyeratibu tukio lote la Ijumaah ya tarehe (17/03/2017).

Makonda anatumika tu wala hana ujasiri wa kufanya yote yale bila baraka za kutoka ofisi kuu ya nchi. Na kuna matukio mengi yamepangwa na yatakuja kutokea na ili yatimie lazima Makonda abaki pale kwa kuwa ni yeye pekee anayeaminika na yuko tayari kutumika.

Na kama mtakuwa hamfurahii ya Makonda basi tambueni kuwa mpaka mkuu wa Makonda aondoke kwanza ndiyo atanyamaza na kukaa kimya la sivyo moto ni uleule.
 
Ajue Mungu wetu yuko macho.Makonda tubu baba.Mungu anamwuana ujue
 
Wa kuwepo milele ni Mungu pekee, muumba mbingu na nchi! Nebukadreza alifanya kufuru kubwa lakini ilifika mwisho! Yuko anaejali wanyonge!
 
He!!! Aisee!!!!!1
 
Nimeacha kuendelea kusoma hapo uliposema amemchapa kibao warioba..maranyingi watu huanza na strong points...kama hiyo ndo strong poinnt...sihitaji kusoma hizo nyingine
 
EWGMS, kesho haiishi na milele ni siku zote daima ndio namaanisha. Leo ndio uhakika wa kila jambo. kesho ni fumbo.
 
Hawezi kuishi milele...lbda atakuwepo kwa kipindi fulani tu

OvA
 
Nimekuelewa Mkuu ila wawili hawa hawatenganishwi kwa sasa na kwa maana hiyo kwao kesho siyo fumbo ni uhakika sababu si rahisi waondoke wote leo.
 
Wa kuwepo milele ni Mungu pekee, muumba mbingu na nchi! Nebukadreza alifanya kufuru kubwa lakini ilifika mwisho! Yuko anaejali wanyonge!
Usihofu hawa washazoea kumkufuru Mungu. Kwanza walijiita kuwa ni Mungu wa dar es salaam then wakapanga kumkashifu.mtumishi wa Mungu kwa kashfa ya uongo
 
Hawezi kuishi milele...lbda atakuwepo kwa kipindi fulani tu

OvA

Tukiamua na kufanya maamuzi magumu hawawezi lakini tukikaa kimya kusubiri miujiza ya Mungu watakaa milele. Si tumeanza kuona sera zinatengenezwa taratibu taratibu tu tukistuka usingizini imeshatoka hiyo tunabaki kupiga mayowe kama Wazimbabwe.
 
Haakuna mwanadamu anayeishi milele hata hyo Mugabe hvyo hvyo tu...
Angalia historia ya kuwa washakhwepo viongozi hadi kujifanya miungu watu lkn walishaondoka duniani!Siku zote biology itakuondoaa tu

Ova
 
tangu lini mtu aliyepiga zero katika taaluma apate uelewa wa kufanya mambo ya msingi katika jamii
 
Back
Top Bottom