Makonda amponda Tundu Lissu, adai bado anaumwa hivyo yawezekana akili yake haifanyi kazi sawa sawa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Ni kuhusu mazungumzo yake ( Tundu Lisu) aliyoyafanya huko Ulaya kupitia shirika la utangazaji BBC.

Makonda amesema maneno haya, nanukuu

''Watanzania wamsamehe kaka yangu Tundu Lissu kwani yeye bado mgonjwa. Sasa kama bado mgonjwa inawezekana kichwani bado mambo hayajakaa vizuri, na ndio maana anahitaji matibabu, na akitoka kule tumuombe Spika amfikishie Milembe, aendelee kumhudumia."
 
Nimempenda Lissu kwa Mambo mawili aliyokwepa Tundu Lissu ni kusema Uongo au kumdhalilisha Mhe Rais. Mengine ni majibu yanayotokana na maswali aliyoulizwa kuhusu madhila aliyoyapata.

Mtangazaji Steven anauliza maswali ambayo media za hapa hawathubutu kuuliza ndo maana Lissu alifunguka; sawa sawa kwasababu ndiye anayeumia.

Na mtu hawezi kwenda Studio na Ushahidi wakati Upelelezi haujafanyika na Lissu hajamtuhumu mtu yeyote moja kwa moja .
Anachofanya kueleza kilichotokea na hatua ambazo zilitakiwa ziwe zimechukuiliwa akisema
Tuiombee Nchi yetu .

Kwa maoni yangu wanaomlaumu walitaka ajifunge kwa kutuhumu mtu moja kwa moja; ili lisije kufanyiwa kazi kitu siku za usoni. Kitu ambacho Lissu alichokwepa asisitiza uchunguzi ufanyike.

Wito wangu tuliombeeTaifa letu



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom