Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,883
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuonesha jeuri waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleao ya Makazi William Lukuvi kuhusiana na eneo la hekari 1,500 alilopewa hivi karibuni kwa kusema ofisi yake inaendelea kujipanga ili kuliendeleza eneo hilo
Hivi karibuni Mkurugenzi wa Hazimio Housing Estate ya Jijini Dar es salaam Mohamed Iqbar alimkabidhi Makonda eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo vya biashara
Baada ya taarifa hizo Waziri Lukuvi alijitokeza na kusema Makonda alidanganywa juu ya eneo hilo na kuwa linamilikiwa na serikali na sio mali ya mfanyabiashara huyo
Mbali na kosa la kudanganya serikali, Lukuvi pia alisema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki Ardhi kinyume cha sheria
Mbali na kauli hizo za Waziri Lukuvi Makonda hakuonesha hali yeyote ya kujali wakati akifungua mkutano wa kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) Jijini Dar es salaam Makonda alisema changamoto za ukosefu wa maeneo kwa wafanybiashara na wajasiriamali zitaondoka kwa kuwa wataalamu wa ofisi yake wanajipanga kuendeleza eneo hilo
Makaonda alisema baada ya kukamika kwa utaratibu wa upimaji eneo hilo litatengwa katika makundi matano ambapo wajasiriamali wa Wilaya zote za Jijini hapa wenye nia za kuwekeza watakabidhiwa maeneo hayo kwa utaratibu utakao pangwa.
Fahari news