YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,992
Raisi Magufuli anataka Tanzania ya viwanda.Viwanda mojawapo ni vya ushonaji.Mafundi cherehani wa Dar es salaam wana uwezo wa kuanzisha kiwanda kikubwa mno cha ushonaji Dar es salaam.Ambacho chaweza shona nguo za kujaza maduka ya jumla na reja reja ya Dar es salaam na zingine kusafirisha nje ya nchi.Nchi zingine kama za Asia ambako zinakotoka nguo nyingi si kwamba zinazalishwa na maviwanda makubwa bali huzalishwa na kushonwa na mafundi cherehani mmoja mmoja na baadaye huzipeleka kwenye Ofisi za CHAMA cha ushirika ambako makontaina ya nguo huuzwa kwa wafanyabiashara wakubwa au huuzwa moja kwa moja nje.
Wanachotakiwa kufanya ni kuunganishwa katika ushirika wa mafundi cherehani Wenye lengo la kuanza ushonaji mkubwa wa kushona nguo kwa ajili ya kuuza badala ya kusubiri mtu aje na kasuruali kametatuka kwenye makalio mtu anataka awekewe kiraka kwa shilingi mia mbili.
Wakiwa katika ushirika ni rahisi mataasisi kama mashule,maofisi nk kuwapa tenda za kushona unifomu za mashule na wafanyakazi wa maofisi kirahisi.Hizi tenda huwa si rahisi kupelekea fundi mmoja mmoja inataka mahali panapoweza zalisha nyingi kwa mpigo.Wakiwa na chama cha ushirika wakawa na ofisi ni rahisi kupata tenda hizo.Kuna mashule unakuta ina wanafunzi elfu tatu shule moja na wote wanataka unifomu.Tenda kama hiyo wakiwa mmoja mmoja hawezi pata
Wakiwa na Chama cha ushirika cha washonaji waweza tajirika haraka kuliko ilivyo sasa.
Pia wakishaunda ushirika waweza letwa walimu toka nchi kama Kongo na ghana wawafundishe ushonaji mzuri wa nguo.
Ghana ni mafundi wazuri mno wa mashati ya wanaume.Nimejaribu sana kushona mashati na mafundi wa Tanzania ni matatizo hata uwape shati kuwa shona kama hii ukamwachia ni taabu tupu.Wakiletewa walimu toka GHANA wanaweza kuwasaidia kuwafunza kushona mashati mazuri ya vitambaa tofauti tofauti ya wanaume.Wakongo pia ni mafundi wazuri wa nguo za fashion mbali mbali waweza watumia kufunza hao mafundi walioko kwenye ushirika.
Mkuu wa mkoa akutane nao awahamasishe kuanzisha hicho chama cha mafundi cherehani ili waanzishe kiwanda chao cha ushonaji.
HAPA KAZI TU
yehodaya123@gmail.com