Adrian Stepp
R I P
- Jul 1, 2011
- 2,764
- 2,600
Wadau, Nimeona nyuzi nyingi sana jukwaani zikizungumzia juu ya mazungumzo kati ya serikali na "wanaume" wa Canada.
Awali kama taifa tulifarijika sana na msimamo uliotolewa na Mh.Rais baada ya uwasilishwaji wa zile ripoti mbili.
Wanasaikolojia hasa wabobezi wa majanga wana kauli mbiu zao endapo unatarajia kitu ama jambo Fulani kwamba 'Be ready, Think ahead, Take care, Brace yourself' hasa katika changamoto mbali mbali za maisha.
Serikali yetu ilitutaarifu juu ya mazungumzo na wale "Wanaume" wa Canada ..Matarajio ya walio wengi ilikua ni kupata mrejesho japo kwa muhtasari wa nini kilijiri na hatua zinazofuata.
Serikali si kwamba haina majibu ila ni suala la muda tuu kwamaana ya si kila taarifa inapaswa kwenda kwa mlaji ( Mwananchi).
Katika misingi ya negotiation kwanza unapaswa kujua nini unataka lakini ni muhimu zaidi kutambua what the other party wants most! Nk
Huenda ni kweli tumeibiwa vyakutosha, tumetambua wapi tulipo chemka..sasa tusonge mbele..wakitupatia hata $5 b hewala maisha yaende na tufunge mkanda upya kwa kuweka sheria na kuziba upigaji kwenye rasilimali..
Tuanze upya! Miaka 3 ya mwisho ya utawala wa awamu ya 4 suala la gesi lilipigiwa chapuo mno..
Hivi unafaham kwamba mpaka 2014 rasilimali ya gesi asilia huko Mtwara ilikua ni ujazo wa futi trilioni 26.99 sawa na mapipa bilioni 4.86 ambayo thamani yake ( kwa wakati ule) ni $ bil.400.81 ambazo ni sawa na Tsh.tril.626.71 ambazo zingeweza kutosheleza bajeti ya nchi kwa zaidi ya miaka 40 mfululizo!!
Tuanzie kwenye gesi..madini kama tunavyo aminishwa kwamba tumepigwa vyakutosha tunaweza tukaweka tu mfumo madhubuti wa uchenjuaji na usimamizi wa mapato.
Nawaza tu kama miaka yote ndg zetu was Nyamongo kule North Mara mgodi uliokua na akiba ya madini ya dhahabu iliyokadiriwa kufikia wakia milioni 36 ambayo imeifanya Tanzania kua ya 3 duniani nyuma ya Ghana na Afrika kusini kwa uzalishaji lakini hata miundombinu ni duni..
Najua wengi wenu hamfahamu kwamba eneo la Mkuju lina hazina kubwa ya madini ya Urani yanayokadiriwa kufikia paundi Mil 182 kitu ambacho inatufanya kama taifa kuwa wa 3 barani Afrika baada ya Niger na Namibia!
Nikweli huenda tuliibiwa, lakini tuki-determine to make a fresh start we can make it!
Ukitupilia mbali sababu lukuki zitolewazo na wanasiasa duniani kote wanapo pigana vita yoyote ile msingi mkuu ni UCHUMI!
TULIANGUKA..TUMEINUKA..TUTAZAME NYUMA ILI TUSIANGUKE TENA..TUSONGE MBELE...KUANZA UPYA SI UJINGA!
Chonde chonde mnaotaka Noah zenu msinitovuge macho!
[emoji115]
Aliye kuambia Matajiri kuliko wote nani!Tanzania yetu siyo tajiri kihivyo kama mnavyoamini, ni kweli tuna Rasilimali za kutosha lkn wengine wanazo pia, hivyo tufute hilo kwamba sisi ndiyo Matajiri Duniani huwo siyo ukweli, ukweli ni kwamba tuna Rasilimali za kututosha kuishi vizuri kama tukiwa makini, lkn hatuna upekee wowote ule!
Mkuu nawe unalijua hili?Tanzania yetu siyo tajiri kihivyo kama mnavyoamini, ni kweli tuna Rasilimali za kutosha lkn wengine wanazo pia, hivyo tufute hilo kwamba sisi ndiyo Matajiri Duniani huwo siyo ukweli, ukweli ni kwamba tuna Rasilimali za kututosha kuishi vizuri kama tukiwa makini, lkn hatuna upekee wowote ule!
Haya mambo ndiyo yanayofanya watu wawe na matarajio ambayo hayapo, semeni ukweli na siyo propaganda kwamba sijui nchi yetu imebarikiwa na Rasilimali klk zote, hiyo ni bullshit, kwani wengine wanazo pia!
I didn’t expect sense coming from, mmmmm!Tanzania yetu siyo tajiri kihivyo kama mnavyoamini, ni kweli tuna Rasilimali za kutosha lkn wengine wanazo pia, hivyo tufute hilo kwamba sisi ndiyo Matajiri Duniani huwo siyo ukweli, ukweli ni kwamba tuna Rasilimali za kututosha kuishi vizuri kama tukiwa makini, lkn hatuna upekee wowote ule!
Haya mambo ndiyo yanayofanya watu wawe na matarajio ambayo hayapo, semeni ukweli na siyo propaganda kwamba sijui nchi yetu imebarikiwa na Rasilimali klk zote, hiyo ni bullshit, kwani wengine wanazo pia!
Huu ndio ushauri wamaana unao lisaidia Taifa
sio wale Vibendera na lichama lao la Vibendera kutwa kuomba mabaya tu kwa taifa!
Ndio maana ikaletwa sheria na Wazungu kupata kiwewe kikubwa kwenya majadiliano.
Tuzidi kumuunga mkono mh Rais wetu
huyu ana nia njema kwa Taifa
Well saidBasi wawe wanasema ukweli kama jamani tumepigwa tuanze upya! sio kukaa kutupigia kelele zisizo Na maana eti tumsifie jpm.....Na kila anayekosoa sio mzalendo!
Sina uhakika kama hata sisi wenyewe kama taifa tuna confidence na ushahidi wetu. Nadhani ndiyo maana tunasita kwenda mahakamani kuhofia kuvuliwa nguo.Hebu justify kuachana na Trilion 425, ambayo ni bajeti ya nchi kwa miaka 14 bila msaada wa senti za wahisani!. Ningekuona una hoja ya msingi ungesema tuwapelekeACACIA mahakamani kwa wizi wote wa madini walioufanya sababu ushahidi wakisayansi tunao!! By Gamba la Nyoka
Tanzania yetu siyo tajiri kihivyo kama mnavyoamini, ni kweli tuna Rasilimali za kutosha lkn wengine wanazo pia, hivyo tufute hilo kwamba sisi ndiyo Matajiri Duniani huwo siyo ukweli, ukweli ni kwamba tuna Rasilimali za kututosha kuishi vizuri kama tukiwa makini, lkn hatuna upekee wowote ule!
Haya mambo ndiyo yanayofanya watu wawe na matarajio ambayo hayapo, semeni ukweli na siyo propaganda kwamba sijui nchi yetu imebarikiwa na Rasilimali klk zote, hiyo ni bullshit, kwani wengine wanazo pia!
Hiyo hoja yako ya kuipeleka serikali mahakamani iandikie bandiko lako..kwanini unamlazimisha mtoa mada afuate unacho taka?Hebu justify kuachana na Trilion 425, ambayo ni bajeti ya nchi kwa miaka 14 bila msaada wa senti za wahisani!. Ningekuona una hoja ya msingi ungesema tuwapeleke ACACIA mahakamani kwa wizi wote wa madini walioufanya sababu ushahidi wa kisayansi tunao!!