Makato ya bank to mobile wallet

pilato93

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
7,942
Reaction score
9,696
Habari za muda huu wakuu,
Twende moja kwa moja kwenye mada leo ni mara yangu ya kwanza kutumia huduma ya nbc mobile sasa nilikuwa na shida kidogo ya buku kumi nikapiga hesabu nikope mpawa kweli nikakumbuka kuwa nina pesa kidogo bank ngoja nivute nimevuta ila makato yao sasa ile huduma ya ussd kwa voda pasipo na salio haifanyi kazi makato yake yaani buku kumi wamemikata buku tatu nzima kweli mwanzo na mwisho kutumia hii huduma toka nbc, yaani roho inaniuma kweli service charges 3000 kwa 10k kweli nbc kuweni na huruma

mpuuzi mpuuzi tu
 
Pole sana
 
Hatare fire


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuweka pesa benki au mpesa ni kupoteza jasho lako.Badala ya benki zikopeshe wafanyabiashara wao wameamua kuchuma lwa kupitia miamala
Nope!
After all, Kukopa ni hiari yako.
Binafsi sioni kama kuna shida ikiwa nitapata emergency inayohitaji kama laki moja hivi nikakimbilia TIMIZA ya Airtel na nikakopa kiasi hicho then ndani ya siku 14 au 21 nikarudisha 115,000/-

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi umeimarika -In Jiwe's voice

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mimi nilikuwa mtumiaji mzuri sana wa kutuma pesa bank kupitia mpesa,, walikuwa wanakata 170 kwa kila elfu 10. Leo hii wanakata 800 Kwa kila elfu 5. Yaani siku hizi mitandao ya simu na mabenki wanafanya mambo ya ajabu sana..

Remember, your mind is greatest asset.
 
Makato ya bank to simu pesa wallet yamekuwa makubwa sana kwa kweli, kuna siku nilihamisha 134,000/= nikajikuta nakwata elfu 5 na kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya makato ni makubwa, lakini vile vile inategemea upo wapi na nini kinakufanya uhitaji hiyo hela.... kama unaweza kopa kwa Riba ya 25% kuokoa maisha ya mtu, utashinwaje kulipa hiyo elfu 5 ili uokoe maisha ya mtu..??

We mtu anaishi MSIMBATI huko Mtwara, nauli hadi ilipo benki anayotunzia pesa zake (MTWARA MJINI) ni 2,500/- na kurudi 2,500/- ( elfu 5 hiyo), mara muda, mara riski za barabarani, jumla itakuwa shilingi ngapi? mara kutokuwa available kufanya mengine..!!
 
It s tru, kabla ya kufanya muaamala lazima ufanye cost benefit analysis, lakini ni muhimu pia kuwa aware na hizi gharama, kuna watu huwa hawajui wanakatwa kiasi gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huduma za bank to simu zimesaidia sana ila BANK/kampuni za simu wanatumia huo mwanya kutupiga fedha,haiwezekani unikate elfu 3 kutoa 10k bank kisha nikienda kutoa kibandani nalimwa tena 1300 yaani kutoa elfu 10 nakutwa nakatwa kama elfu 5,huu ni wizi mkubwa,BOT/TCRA inabidi wailngilie kati,tunawafaidisha wahindi huku waTZ wanaumizwa.
 
Nimekoma mie situmii kuweka wala kutoa yaani ukitumia atm tofauti na yao wanakulima 3600 yaani mpaka roho inauma ukiweka ndani pesa vijana wanaweza kukuotea basi tabu tupu

mpuuzi mpuuzi tu
 
Haya mabenki mie nilishasema ni majambazi sana. Yani mara 10000 utie hela yako MPESA ufanye kama unaitunza tu huko amna kuitoa. Ili maumivu yaje siku unapoitoa yote labda una draw million nzima!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…