Mkuu,
Sijui niseme unawapenda sana hawa watu wa vijijini au ndio unajaribu kuwaamsha?
well, Makao makuu ya serikali huwa mijini, serikali nyengine hujenga miji mipya kwa ajili ya makao hayo, kama TZ, Dodoma, Abuja, Nigeria, Brazilia, Brazil....mako makuu ya ofisi zote huwa mijini, makanisa na misikiti mikubwa na ya kuvutia huwa mijini.....hata mimi huwa ninajiuliza masuali mengi sana kuhusu hali hii....yaani dhiki na shida zote kwa wanavijiji.....halafu hukumbukwa kwa ziara fupi za viongozi kama ni wa serikali au kidini...halafu wanatakiwe watoe sadaka au walipe kodi na waamini kuwa mungu yuko pamoja nao wakati wajanja wanatanua mijini...
Mkuu haya mambo ni vituko tu,tena katika nchi zote!!!
Wenyewe husema,"penye fungu ndipo panapopata nyongeza!"
Hao wa vijijini waendelee kupiga jembe lao na wasubiri kuletewa maendeleo...hapo katikati pana mambo..yaweza wakakabiliana na mauti kabla ya maendeleo kuwafikia au wafungashe virago kuelekea mijini na wao wakabane na wajanja huko huko.