Makamu wa Rais azitaka nchi za SADC kupambana na viumbe vamizi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka nchi za SADC kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na viumbe vamizi ambao ni changamoto kubwa katika nchi wanachama kwacsni wamekua na athari kubwa katika mazingira na uchumi.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa Nchi za SADC amesema kuwa suala la viumbe vamizi ni tishio kubwa kwa mazingira kwani linathari kubwa.

Amesema kuwa Viumbe vamizi ni hatari kwa ustawi wa Mazingira, hivyo nchi wanachama zinatakiwa kuwa na mkakati wa pamoja ambao utawezesha kuwatokomeza ili wasilete madhara makubwa na kuathiri mazingira

Kuhusu vivutio vya utalii, amesema nchi za SADC zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambapo Sekta ya Utalii inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi wanachama kwa mjibu wa takwimu sekta ya utalii inachangia dola za kimarekani bilioni 56.3 ambazo ni sawa asilimia 8.2 % ya ihifadhiwe pato gafi

Amesema kwa upande wa Tanzania Sekta ya Utalii imeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi ambapo mwaka 2018 sekta ya utalii ilichangia dola za kimarekani bilioni 2.4

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dokta Hamis Kingwangala, amesema jukumu kubwa la mkutano huo ni kuridhia mapendekezo yaliyowasilishwa na wataalamu ambayo yanalinda maslahi ya Jumuia hiyo na majadiliano yalijikita katika kupima utekelezaji wa sera na mikakati mbalimbali .

Waziri Kingwangala amesema Itifaki ya usimamizi wa misitu na mkakati wa misitu, itifaki ya SADC kuhusu maendeleo ya utalii ,program ya maendeleo ya utalii naitifaki ya SADC ya usimamizi wa Mazingira kwa maendeleo endelevu na mkakati wa mabadiliko ya tabia nchi ,program ya SADC ya kupambana na kuenea kwa jangwa.

Wakizungumza katika mkutano huo Kamishina wa uhifadhi wa Misitu,TFS ,Prof. De Santos Silayo na Kamishina Mhifadhi wa Mamlaka ya Wanyama Pori (TAWA), Dkt James Wakiban wamesema...

IMG-20191025-WA0027.jpeg
 
Back
Top Bottom