Makambako standi ni madimbwi tu

Mangandula

Senior Member
Nov 30, 2011
184
37
Nipo ndani ya basi natoka mbeya naingia makambako standi nakaribishwa na madimbwi! Hivi jamani hivi si vitega uchumi vinavyoingiza fedha kila iitwapo leo? Je viongozi hamuoni kama kuna umuhimu wa kuikarabati hii standi ili mpate malipo ya haki? Mbunge uko wapi? Diwani wa eneo hilo uko wapi? Hakika hii ni kero kwa walipa kodi na abilia kwa ujumla. Nimeambiwa na wenyeji kuwa kila wakipiga kelele au kutoa maoni kuhusu hii standi wanapata misukosuko! Mara wataambiwa wao ni wapinzani, pia nasikia waandishi wa habari wengi wameenda eneo la tukio na kuhoji lakini pindi wanapoondoka tu cha moto lazima wakipate. Leo mjaribu kuwasumbua muone! Badala ya kushughulikia matatizo yanayowakabili wananchi mnawanyanyasa wapiga kura wenu! Shughulikieni tatizo la maji, barabara na watendaji wanaotafuna fedha za maendeleo.
 
Nipo ndani ya basi natoka mbeya naingia makambako standi nakaribishwa na madimbwi!.

Haaa! Mara hii upo Makambako! Umetoka Mbeya Saa Kumi na Mbili asubuhi au saa Tisa Usiku? Nyie ndio wale ambao madereva wanakimbiza magari kwa kasi mnashangilia alafu gari ikipata ajali mnaanza kulalamika, Ooh dereva alikuwa anaenda kasi, Ooh gari mkweche nk! Mwambie dereva apunguze mwendo! Ilitakiwa muwe mpakani (Mbeya & Iringa) kwa muda huu na sio Makambako!

Mangandula: Makambako cha mtoto ungesogea kidogo hadi Njombe ukaangalia stendi ya hapo ndo ungezimia kabisa. Uwezi amini kama ni makao makuu ya mkoa mpya.ni juzi juzi wananchi walipiga kelele wakawa wamemwaga kifusi ambacho sasa hivi mvua ikinyesha inakuwa ni uji mtupu(tope), hayo ndo maendeleo ya miaka 50 ya uhuru.
 
Hiyo ndiyo Happy nation saa 2:05 tupo stand makambako.
 
Mangandula: Makambako cha mtoto ungesogea kidogo hadi Njombe ukaangalia stendi ya hapo ndo ungezimia kabisa. Uwezi amini kama ni makao makuu ya mkoa mpya.ni juzi juzi wananchi walipiga kelele wakawa wamemwaga kifusi ambacho sasa hivi mvua ikinyesha inakuwa ni uji mtupu(tope), hayo ndo maendeleo ya miaka 50 ya uhuru.

Kumbe ugonjwa huu upo sehemu nyingi ati! Hata makao makuu ya mkoa stand ni tope? Kuna umuhimu wa watumiaji wa hizi stand kugoma kulipa ushuru ili wajue umuhimu wa kukarabati eneo husika. Hata stand ya mafinga nako hakujakaa sawa.
 
Back
Top Bottom