Makamba: Zaidi ya ekari 2500 zinateketea kila siku

Majs

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
232
515
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema zaidi ya ekari 2500 za hifadhi ya mazingira nchini zinateketea kila siku na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuharibu vyanzo vya maji.

Makamba ametoa kauli hiyo Jijini DSM wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa itafanyika wilaya ya Butiama mkoani Mara ili kuenzi mchango wa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika utunzaji wa mazingira.

Makamba.jpg
 
Waweke sera nzuri tutoke kwenye kutumia kuni na mkaa... watu watumie gas, makaa ya mawe, na mkaa wa kutengeneza bila kutumia miti.
 

January Makamba aeleza kuwa hatutaushinda umasikini kama kasi ya uharibifu mazingira itaendelea. Maendeleo na utunzaji wa mazingira yanaendana pamoja.
 
Huyu naye kutwa anaongea lakini hakuna mikakati ya kuokoa mazingira zaidi ya porojo, punguzeni gesi watu watumie gesi mpaka vijijini.
 
Back
Top Bottom