Uteuzi wa January Makamba una walakini. Rais alipaswa alione hili kwamba kuna conflict of interests katika wizara hii ambayo pamoja na mambo mengine ni kuyadhibiti makampuni ya simu ikiwemo Vodacom. Dada yake Mwantum alitumia nafasi yake kupitia Vodacom Foundation kumwandalia mazingira ya ushindi jimboni kwake Bumbuli. Shule zilijengwa na vifaa vya elimu vilipelekwa kwa mgongo wa vodacom social responsibility, hata zahanati zilipata ufadhili wa vodacom. Je January ataweza kudhibiti makampuni ya simu yanayokiuka taratibu za kodi etc likiwemo la dada yake la Vodacom?