Makala: Makonda kafa kisiasa, hawezi kufufuka kama Magufuli asipokuwa madarakani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
NAWEZA kusema, bila shaka yoyote, kwamba mwisho wa kisiasa wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, umefika. Kwa namna ilivyo sasa, hawezi kufufuka kutoka katika wafu.

Ataendelea na wadhifa wake alionao sasa kwa sababu Rais John Magufuli ameamua hivyo. Uhai wake wa kisiasa uko katika viganja vya mikono vya mtu mmoja.

Lakini, kwa walio wengi, uhalali wake wa kisiasa umepotea. Si yule Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na wala si Makonda aliyeanza kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Naandika hivi kwa uchungu kwa sababu Makonda ni kijana mwenzangu. Katika hali ya kawaida, namna pekee ya vijana kuaminiwa kupewa madaraka makubwa, ni kwa wale waliopewa fursa hizo kuzitumia vizuri.

Kuna watu walikuwa na dhana kuwa Makonda ni kijana mdogo sana kupewa wadhifa wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Baada ya yaliyotokea, imani yao hiyo imekolezwa kuwa mkoa huu unahitaji watu wa aina na umri fulani.

Lakini, Makonda ni mfano mmoja wa wanasiasa vijana waliopewa fursa katika nyakati za kuanzia utawala wa Jakaya Kikwete na Magufuli ambao wameonyesha kuangusha wenzao.

Katika taifa lolote lile, ni jambo la mbolea kuona nchi ikiwa inaongozwa na watu wazima na halafu wakionekana vijana walio tayari kushika hatamu wakati zamu yao itakapofika.

Inasikitisha kwamba wengi wa vijana waliopewa nafasi wamezitumia vibaya kiasi kwamba wengi wao wamekuwa na maisha mafupi kisiasa.

Kuna wanasiasa ambao umaarufu wao umedumu kwa miaka mitano tu. Wengine mitatu na wengine wamedumu kwa mwaka mmoja tu! Inaacha maswali mengi kuhusu mustakabali wa taifa letu.

Kwa sababu ambazo si rahisi kuzielewa, wamewahi kuibuka wanasiasa vijana na wenye uwezo lakini wakakubali kuwa wapambe au wapiga debe wa wanasiasa wengine wakubwa au mashuhuri.

Vijana hao walifungamanisha hatma zao za kisiasa na za wakongwe hao kiasi kwamba anguko la ‘baba au wazee’ hao wa kisiasa, lilimaanisha anguko la pia.

Wakakubali kuwa wabeba mikoba. Wakaacha kufikiri kwa niaba yao. Wakawa wanaacha akili zao kwenye malango kila wanapoingia kwenye nyumba za vigogo hao.

Wengine, baadhi wakiwa na taaluma zao walizosomea, wakaacha kufanya kazi za kisomi na kujiingiza katika ‘kazi ‘ za kijinga ikiwamo ukuwadi, ulozi na uvuvuzela wa wakubwa fulani.

Kuna wanasiasa wawili vijana ambao nadhani wanasiasa vijana wanaochipukia wanapaswa kujifunza kutoka kwao kama wanataka kubaki katika siasa kwa muda mrefu.

Chukulia mfano wa Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe. Alipomaliza Chuo Kikuu, kwanza alifanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali.

Alitumia taaluma yake. Alihangaika. Alijua nini maana ya kutakiwa kwenda kazini kila siku wakati mshahara hautoshi. Alijifunza ubunifu. Pengine alitengeneza marafiki waliokuja kumsaidia baadaye.

Mwingine ni January Makamba. Alipomaliza Kidato cha Sita, alifanya kazi katika makambi ya wakimbizi. Akazifahamu shida za wananchi. Akajua ubaya wa vita. Akatengeneza marafiki wa namna yake hapo.

Alipomaliza Chuo Kikuu, January aliajiriwa na Wizara ya Mambo ya Nje ambapo alifanya kazi kama vijana wengine. Huyu hakuibuka tu katika siasa, alitumia kwanza taaluma yake.

Ni kama Barack Obama wa Marekani. Huyu alifanya kazi, tena kwa kujitolea kusaidia wasiojiweza kule Chicago. Akajua shida za watu. Akazoea kuishi kwa kipato chake.

Paul Makonda, na wanasiasa wa aina yake, hawajapitia maisha haya. Kuondoa siasa, Makonda hajawahi kufanya kazi yoyote ya kuajiriwa, hata kama ni mhitimu wa Chuo Kikuu.

Baba wa Taifa, Julius Nyerere, alikuwa mwalimu kabla ya kuingia kwenye siasa. Benjamin Mkapa alikuwa mwandishi kabla ya siasa. Mzee Ali Hassan Mwinyi alikuwa mwalimu. Hata Kikwete alianzia kuajiriwa katika ngazi za chini za chama.

Nina shida na viongozi vijana wa taifa letu ambao siasa kwao ni ajira. Nadhani huu ni miongoni mwa mwanzo mbaya ambao vijana wa sasa wanajitengenezea wenyewe.

Mwanadamu anatakiwa kuwa kwanza na malengo ya kufanikisha katika taaluma yake. Maisha ya kisiasa ambayo hayana msingi wa kazi zilizofanyika kabla, huwa hayadumu.

La pili ambalo ni muhimu kwenye muktadha huu wa vijana ni suala la kujitambulisha binafsi kama mwanasiasa. Ili udumu katika siasa, ni lazima ujipambanue kwa jinsi ulivyo na si kwa kutumia mgongo wa mtu mwingine.

Hapa tena, narejea kwa January na Zitto.

January ni mwanafunzi wa kisiasa wa Kikwete. Kama angetaka, angejibananisha naye au kuwa kama vijana wengine walioangukia kwa Edward Lowassa. Angebaki kuwa mpambe tu na ingetosha.

Lakini, alipopata ubunge na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, January alifanya kazi nzuri kuwa mwiba hata kwa serikali ya Kikwete yenyewe.

Hata alipopandishwa na kuwa Naibu Waziri, hakuna tena aliyesema kuwa amebebwa. Leo hii, anatambulika kama January zaidi na si mtoto wa Yusuf Makamba au kijana wa Kikwete. Amejipambanua uwezo wake mbele ya jamii.

Ni sawa na Zitto. Ni wazi kwamba Freeman Mbowe ana mchango wake kwenye kumpa fursa ya kisiasa. Lakini alipoipata, akajitutumua na kusimama mwenyewe. Kama angetaka, angebaki tu kuwa kama kijana wa Mbowe; kama walivyo vijana wengine.

Ameibua mambo yake mwenyewe, ametafiti mambo, ametafuta marafiki zake na kujijengea uhalali wake wa kisiasa binafsi. Ndiyo maana ameweza kutoka Chadema na anaishi kisiasa hadi leo.

Kuna wanasiasa vijana na wenye akili lakini wamekubali kuwa ‘vijana’ wa Maalim Seif, Lowassa, Augustine Mrema na wanasiasa wengine maarufu. Matokeo yake, hatma yao ya kisiasa imefunganishwa na vigogo hao.

Somo kutoka kwa Makonda na vijana wengine waliodumu muda mfupi katika siasa liko wazi; kwanza lengo liwe kufanya kazi ya kitaaluma inayoonekana na kisha matamanio ya kisiasa yafuate mkondo. Na wakati huo utakapofika, wasimame kwa miguu yao.

FaceTwiGoWha
 
Kucheza siasa za Bongo ni rahisi sana. Nani alikua adui mkubwa zaidi ya EL?
Nani alitukanwa kama Nnape?
Nani alikejeliwa kama JK?
Nani aliwahi kumpenda shibuda?
Nani alikuwa rafiki wa Lembeli?
Lini Bulaya alikuwa na mashabiki wa kumtetea?!

Bongo unaeza kujijengea heshima kwa tukio la dakika 20 tu.
 
Binafsi kimtazamo sidhani kama Makonda ni mwanasiasa.

Na sijawahi kumchukulia kama mwanasiasa zaidi ya kuwa ni kijana aliyepata nafasi ya kupewa uongozi.

Ukitazama na kufanya tafakari kwa makini, Zitto sawa na mwanasiasa, January ni mwanasiasa pia so be to the likes kama akina Nape ni mwanasiasa. Hawa ni wanasiasa kwa sababu tu walipita katika mikono ya wanasiasa wakapata mafunzo/malezi ya kisiasa thats why wana political sentiments with them.

Makonda ni kama ana leadership sentiments with him
He is just a leader NOT a politician. Sidhani kama Makonda anaweza simama mbele ya halaiki akajenga hoja na kuko~convience watu politically zaidi ya amri za hapa + pale.
 
Dawa zinasumbua
Kwanini cheti fake kionekane baada ya kutaja wenye pesa ya ngada
 
Kama Edward Lowassa siku hizi ni mungu huko ukawa, hakuna kisichowezekana hapo bavicha
 
Dr Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibiwa ujauzito akiwa Arusha wakati wakitetea Chadema.

Lakini alifukuzwa dakika za mwisho na chama kuuziwa Lowasa.


Leo wako bize kumhurumia Nape!!
 
Kama Nape leo ni shujaaa hata Makonda anaweza kuja kuwa shujaaa.....ishu ni kuwapendeza tuuuu
 
Kuna MTU kaambiwa na nape atoe kitambulisho akatoa bastola ..,....sasa sijui angeambiwa atoe vyetii si angetupa Bomu......pwAaaaaa....


Mwafwaaaaaaa
 
Back
Top Bottom