The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,950
- 12,549
John P. Magufuli ni mgombea urais kupitia CCM hajui chama chake.
Baadhi ya wakosoaji wake wanaishangaa CCM iliyomteua kugombea urais wakati hajawahi kushika hata ubalozi wa nyumba kumi ndani ya chama hicho.
Kibaya zaidi, wanasema hakuwahi kujiandaa kuwa kiongozi mkuu wa nchi au chama hicho.
Kwa utaratibu wa waliojiwekea CCM, anayechaguliwa kuwa rais ndiye hatimaye huwa mwenyekiti wa chama hicho; hivyo ikitokea Magufuli akashinda, anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa CCM.
Kauli anazotoa jukwaani, kwamba anataka kuifanya "Tanzania ya Magufuli" kuwa ya viwanda, hazipaswi kutolewa na mtu aliyekuwa waziri katika serikali iliyoua viwanda.
Ni kauli isiyopaswa kutolewa na mgombea wa urais wa chama ambacho kiliuza viwanda zaidi ya 400 kwa wageni na baadhi ya wenyeji ambao walishindwa kuviendeleza.
Kwa mantiki hiyo, vijana wa Tanzania hawawezi kukubaliana na Magufuli kwamba atajenga viwanda ili kuwatengenezea ajira, wakati wanajua naye ni mmoja wa wauzaji na wauaji wa viwanda hivyo.
Kila anayemsikiliza na kumtazama Magufuli jukwaani anajisemea kwamba "huyu bwana anajiongopea."
Magufuli wa CCM ile ile iliyoua viwanda, hawezi kuwa mtu sahihi wa kuwaaminisha watanzania kwamba atajenga viwanda.
Heri Magufuli angekuwa mgeni. Ni mwenyeji wa siku nyingi, akiwa na miaka 20 ya ubunge na 15 ya uwaziri katika serikali za awamu ya tatu na nne.
Katika uwenyeji wake huo, Magufuli ndiye alishawishi serikali, kupitia Baraza la mawaziri, kuuza nyumba za serikali kiholela na kuingiza taifa hasara kubwa.
Kwa hiyo, muuzaji wa nyumba na muuaji wa viwanda vya serikali, hawana tofauti. Yeyote nwenye akili timamu, hatakubaliana na Magufuli kwamba yeye ni Mwana CCM tofauti na wenzake.
Kama atapenya, urais wa Magufuli hauwezi kuwa tofauti na urais wa Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
Watatofautiana kwa kauli na mbwembwe za kunadi Sera zao, lakini malengo ya Mkapa, Kikwete na Magufuli ni yale yale. Hatuwezi kuwaamini.
Tunajua CCM hawajiamini tena. Wanashindwa kuomba kura kwa kutumia chama chao. Wameamua kutumia Magufuli kama kete yao ya mwisho. Lakini wanasahau kuwa Kete yao ya mwisho ya CCM ilikuwa ni Kikwete, sio Magufuli.
Kikwete alipoingia katika kinyang'anyiro cha kusaka urais mwaka 2005, CCM ilikuwa inakaribia kubomoka.
Aliingia kama "tumaini jipya" akajinasibu kwa kauli mbiu ya "Maisha bora kwa kila mtanzania". Watanzania wakadanganyika, wakamwamini.
Miaka 10 iliyopita imeonesha watanzania kwamba CCM haiwezi kuaminika tena. Maisha bora yamegeuka kuwa maisha duni. Kikwete ameshindwa kuibadilisha CCM, badala yake CCM ndiyo imembadilisha yeye.
Leo hii matumaini ya watanzania yametoweka.
Lugha inayozungumzwa sasa ni mabadiliko. Na mabadiliko ya kwanza wanayoyataka watanzania ni kuiondoa CCM madarakani, mengine baadaye.
Hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kumwona Magufuli kuwa mtu mwenye nia njema ya kuleta mabadiliko eti kwa kuwa naye anailaumu serikali ya Jakaya Kikwete kwa kujenga shule chini ya kiwango, kwa kuwa na hospitali zisizo na dawa, kwa kuwa na barabara zinazobomoka kabla ya muda wake.
Matatizo haya ni mazao ya serikali na sera za CCM ya Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa, Jakaya Kikwete na Magufuli wao.
Kwa hiyo kama tunatafuta kiongozi mkuu wa nchi wa kuibadilisha Tanzania, hawezi kuwa Magufuli.
Si kwa kuwa Magufuli ni mtu mbaya. La hasha!. Ni kwa sababu yumo ndani ya mfumo uleule ulioididimiza nchi hii, na anataka kutumia mfumo huo huo kuleta mabadiliko. Hawezi!!
Na alivyo mjanja, baada ya kubaini kuwa watu wanataka mabadiliko kwa ari kubwa, Naye aneanza kusema eti ataleta mabadiliko!!
Lakini waelewa wameshasema CCM ni gari bovu. Kama dereva anataka kuliondoa hapo lilipo, lazima atoke nje ya gari, asukume.
Frederick Sumaye na Edward Lowassa, mawaziri wakuu wa zamani na baadhi ya makada maarufu wa CCM, baada ya kukutwa na masahibu makubwa ndani ya chama hicho, wameona hili na kufanya uamuzi wa kushuka ili wasukume gari wakiwa nje.
Ndiyo maana umma wa watanzania umeamua kuwakubali na kuwaunga mkono. Ndiyo maana wameonekana mashujaa kuliko Magufuli.
Wananchi wanamshangaa Magufuli kwa kubaki ndani ya CCM huku akiimba "mabadiliko". Watanzania wa leo, wameshaamua kuwa mabadiliko ndani ya CCM hayawezekani.
Magufuli amebaki na kundi linaloamini kwamba wanaweza kuleta mabadiliko wakiwa ndani ya CCM. Hawaoni njia. Hawajui waendako. Hawasikii sauti za wapenda mabadiliko. La labda ndiyo maana wanatutukana na kutuita wapumbavu na malofa!!
Sasa umefika wakati, wapumbavu na malofa wanafanya uamuzi utakaotengeneza upya mustakabali wa Tanzania.
Malofa wanataka Tanzania mpya, isiyoongozwa na CCM. Ni Tanzania. Si ya Magufuli, kwa sababu wameshaamua.
Tanzania ya Watanzania malofa, wenye nchi yao, wanataka mabadiliko ambayo Magufuli hayaelewi, na hayawezi kuyaleta.
Kama Magufuli anayasema kutoka moyoni, basi nataka niamini kuwa hakijui chama chake. Hajui kuwa kinamtumia kutafuta kura, na zikishapatikana kitamziba mdomo na kumfunga mikono na miguu asifurukute kabisa!
Rais na mwenyekiti asiyejua chama chake, hawezi kukisukuma kuleta mabadiliko tunayoyapigania. Angekuwa mpiganaji wa kweli, angekuwa aneshajiondoa CCM ili ajiunge na wapenda mabadiliko.
Kama alidhani kuwa tutakubaliana na porojo za mabadiliko ndani ya CCM, ajue kuwa zamu hii hatudanganyiki.
Magufuli anajindanganya. Wanaotaka kuleta mabadiliko; wanaopigania mabadiliko wameshahama kambi, wako upande mmoja dhidi ya CCM!.
Wanaopigania mabadiliko wanajulikana. Magufuli si mmoja wetu!
(Source: Gazeti la Mawio; Septemba 10 - 15, 2015 ; Mwandishi akiwa Ansbert Ngurumo, mgombea ubunge (CHADEMA/,UKAWA jimbo la Muleba Kaskazini, mkoa wa Kagera)