Kurudi nyuma haimaanishi kujisalimisha. Ni kujipanga upya twendeni tukajipange sasa.
Na: Fundi Mkuu (facebook).
Makala haya ni muunganiko wa kusitisha habari zimhusuzo BEN katika Ukuta Huu, na Kuwaasa vijana juu ya safari tuiendeayo, safari imejaamiiba hivyo vema kujipanga upya. Nasema nasitisha kuandika habari zimhusuzo BEN, na kupunguza kuwakosoa wasiopenda kukosolewa (Kama si kuacha kabisa)
Siku 52 zimepita, leo ni Siku ya 53 tangu siku inayosadikiwa kupotea kwa BEN. Alipoandika Makala yake Malisa kusitisha habari zinazomhusu BEN niliumia sana, zaidi ya yote nikajifikiria mengi. Hatimae siku imefika nami Leo kuwatangazia wafuasi wa UKUTA huu kuwa leo ni siku ya mwisho kuweka mabandiko ya habari za BEN hapa unless itakapolazimika kufanya hivyo.
Ukuta huu umekuwa ukiandika makala mfululizo za kumhitaji BEN akiwa Hai. Kwa hali ilivyo na namna ambavyo nimefanya juhudi zangu binafsi kutafiti na kupitia baadhi ya viongozi, nimejiridhisha kuwa suala la BEN ni Nadharia. Mengine yote tunayoyahisi nasema ni nadharia na hisia ambazo hazina matokeo mubashara. Nami niseme tu kuwa kumtafuta BEN kunahitaji akili za ziada.
Kwa kuwa Jamhuri ambayo inapasa kuwalinda Raia wake na ndiyo ilipasa vile vile kumlinda BEN, na bahati mbaya kuwa hadi sasa haijatoa taarifa yo-yote kuhusu alipo kijana huyu mlipa kodi. Yawezekana wanaendelea kumtafuta au wanajua alipo hivyo ipo siku watatueleza ukweli.
BEN ni mwanadamu, anao mwili una nyuma, na damu, lo-lote baya kwake ni maumivu, Wazazi wake na nduguze tukiwemo marafiki zake tumelia Sana, Lakini Sasa umefika wakati nalazimika kusitisha rasimi kama ambavyo wamefanya makamanda wengine Malisa GJ na Yericko Nyerere.
Nakumbuka Kauli moja aliyopata kuitoa Lissu katika moja ya mabandiko yake kwenye WhatsApp, kauli ambayo iliniumiza sana, lakini leo nimeielewa, alisema kwamba “Wengi wameumizwa, na Ben anaweza asiwe wa mwisho kupotea au kuumizwa, lakini hatuwezi kurudi nyuma, lazima tusonge Mbele……..”
Niseme tu kuwa, ni bahati kuwa kwa BEN watu wanapiga kelele na kumtafuta mitandaoni. Si ajabu wapo wengi sana wamepotea kwa mtindo na aina kama hii ya BEN. Mungu tuhurumie…
Nasema kwa kuwa hakuna mwenye taarifa kamili, sahihi na Rasimi kuhusu BEN, basi hatuna budi kujipanga upya, tutamtafuta BEN kwa namna nyingine. Na waliohusika siku moja Mungu atawadhihirisha nao watamwachia either akiwa Hai, mfu au akiwa ameoza.
= = = = = = = = = = = = = = = = = = =
Kwa upande mwingine nampa pole Mbowe na uongozi wake, nawasihi vijana msimshambulie Mbowe juu ya suala hili la BEN.
Tujue Mbowe ni binadamu anajua ugumu wa suala hili, ikiwa pengine kwa hisia unayetaka akusaidie kumtafuta ni miongoni mwa unaowahisi. Ni mtihani. Tutiane moyo badala ya kugeukiana. Sidhani kama katika hivi vita adui yetu ni Mbowe wala Sosopi wala katibu mkuu Mashinji. Adui ana mbinu nyingi kuwapumbaza.
Hili la BEN nalifananisha sawa na watu walioko vitani kupambana na adui. Ghafla mmoja wa wapambanaji anapotea, sasa kama mwenzenu kapotea msituni tena una kila dalilili zinazoonesha kuwa pengine adui yako ndiye amemchukua anaye, mnaachaje mapambano na kuanza kufokea viongozi wenu eti kwa nini mwenzetu hapatikani na kwamba mnakatishwa tamaa.
Ni nani atapona mwisho wa siku katika mapambano hayo? Pengine viongozi wamejua wakaamua kutokuimba wimbo ambao adui ameamua kuwaimbisha ninyi vijana. Utulivu wetu Utapima busara zetu na Kumnyima Adui Ushindi! “Ndugu tupunguze Kuwa Composed……!!!
Natamani tungepata Chuo cha kupunguza maneno na kutafuta mbinu za kukabiliana na Adui anayepiga hatua katika mabega yetu…..!”
Kama Vijana tuape kusaidia kulinda Nchi na Taifa letu wakati wa Dhoruba na Utulivu! Kila mwanaharakati anajua fika kuwa tunapita kipindi kigumu ki-ushindani kuliko wakati wowote ule uliopata kutokea, japo nafasi ni nyeupe kama tu “Nyufa za hisia” hazitapaliliwa kwa maslahi ya Adui yetu! Jamaa wamezidiwa kwa hoja, sasa ni mabavu tu
Nanyi mnajua tabia ya mtu Mgomvi anapozidiwa hoja linalofuata ni nini? Nawasihi vijana na wapambanaji wengine tuchukue tahadhari na kutiana moyo, tusithubutu kumtunishia misuli mtu aliyejipanga kukuumiza, zaidi ya yote tudhibiti mashambulizi yasitudhulu, na njia pekee ni kunyamaza kimya. Ukinyamaza kimya, atakosa la kukufanyia, huku ukijipanga upya.
Wewe nyamaza tu, endelea kunyamaza na kukaa kimya, kuna wakati unayehisi ni adui yako ataona aibu na kubaki kufanya vituko tu badala ya kutoa huduma impasayo kuitoa. Nawaasa Vijana wenzangu isikieni hii sauti haitawadhulu kitu kunyamaza. Nyamaza kijana mpenda Nchi yako, siku yaja watachanganyikiwa hata wa kumkamata watakosa watabaki kufanya vituko. Wakati utakuja wa kusema, tutaongea kwa kiburi na Sauti kuu…..!!
Kwa kufanya hivyo, si kwamba tunazila na kuacha kokosoa, bali tunaamua kurudi nyuma kujipanga upya namna ya kuikabili hali tunayoipitia. Haivutii wanaharakati kufanya yao. Inaogopesha, Inatisha. Haipasi kupungua wengi. Mwana Harakati makini ni yule anayruhu “Kupngua” mara tu baada ya kufikisha Ujumbe wake na mapambano yake kueleweka kwa wale anaowapigania. Ref Malcom X, Martin Luther, Bob Marley, Steve Biko, Patrice Lumumba, n.k
= = = = = = = = = = = = = = = = = = =
Mapendekezo Nini kifanyike:
Namna pekee ya kutekeleza hayo niliyaainisha hapo juu is Just to shutup and sew our mouth
1) Usikosoe wala kuhoji hatungependa kukutafuta bila mafanikio Jitahidi sana kuchunga ndimi zako katika zama kama hizi. Usiseme ukweli hadharani wenyewe hawataki. Tujitahidi sana kuwa wanafiki hata kama ukweli unajulikana, Usiuseme ukweli, wala usipende kuhoji hadi wakati utakapofika.
2) Kama hupendi kunyamaza. Basi sifia tu hata kama unakufa wewe sifu. Hata kama hupendi, wewe endelea tu kusifu, hadi koo likukauke, ikiwezekana, piga makofi na vigeregere vingi, kama ambavyo walifanya watu wa Kaitaba wakati Mzee anawananga na majanga yao, hata vijiji vyao ikiwemo Katerero
3) Unapopatwa na janga usieleze kwa watawala, maana hilo ni lako, Kila mtu ahakikishe anaubeba Msalaba wake. Hakuna Serikali inayoshughulikia majanga katika dunia hii. Kuhusu elimu itolewayo, tusiihoji sana ili mradi tu watoto wanasoma bureee, muhimu watoto wote wasome bureee, si unajua Serikali inatumia bil 18.5 kwa mwezi?
4) Dumisha Umoja na Amani hata kama ni kinafiki. Tuendelee kuhubiri Amani hasa misikitini na makanisani. Tuendelee kupandikizana “ujasiri” kwa dini zetu, kwa Imani zetu za dini, kwa itikadi zetu za kisiasa, kwa makabila yetu, na ikiwezekana tuendelee kuweka zile speech za Nyerere huku tukiendelea kuunga hoja ya kuzungusha moto nchi nzima. Bila kujali kuwa ni laana. Soma Isaya 50:11
5) Katika kipindi hiki cha Ukame, hakikisha unawasaidia wazee wako kijijini wasije kufa njaa. Hata kama tunajua fika kuwa ndio wametusababishia haya yanayotupata leo, kwa kutuona sisi “Magaidi tunaopenda vita” Leo hii njaa inakuja kwao, hakuna anayewajali. Beba huo ni msalaba wako, wasaidie ipasavyo
6) Mwisho, hakikisha unalipa kodi hata kipato chako cha mwisho bila manung’uniko, ili ikiwezekana, urudipo nyumbani ukose hata pesa ya kununua Nepi za wanao. Lipa PAYE, nenda ATM kakatwe kodi, ukituma kwa wazazi katwa kodi, na mzee mwekee ya kutolea itakayokatwa kodi. Wewe usijali endelea tu, ndipo Ufalme wa Taifa hili utakufaa
Watakosa wa kumkamata, wala wa kumpiga, ndipo hapo tutashuhudia kipindi cha kufanya vituko na wale wanaotubeza wataungana nasi ili kujitetea, wakati sasa wanafurahia maumivu yetu. Kitakuwa kipindikigumu kwao wanaoshangiliwa leo. Naingoja siku hiyo………!!!
#BRING_BACK_BEN_ALIVE
By Fundi Mkuu
8th January, 2017