Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,421
Jana niliandika makala moja iliyosema, UVCCM niwazalendo au ni wahalifu wa Taifa hili? UVCCM ni wazalendo au wahalifu wa Taifa hili?
Naam, leo nimeonelea niichambue makala hiyo kwa urefu na ufafanuzi zaidi ili kuwasaidia wale ambao hawakuelewa vizuri malengo ya mada ile. Ni ukweli usiopingika kwamba Vyama, serikali na wanasiasa huundwa na kutoweka,
Lakini nchi ipo na itakuwepo daima, hivyo vyama vyetu vya siasa kwanza ni maslahi yetu, ndipo mengine hufuata...
Mwanaharakati ni mzalendo lakini kwa nadharia na vitendo hawezi kuwa kiongozi, ukimpa uongozi maranyingi hufeli, kwasababu msingi wa uongozi wa nchi kidunia umewekwa chini ya vyama vya siasa ambavyo kwanza ni maslahi ya kisiasa kwanza,
Mfano rahisi ni Che Guevara, baada ya uhuru wa Cuba alipewa uwaziri wa fedha, akaachia na kuamua kurudi msituni kudai uhuru wa mataifa...
Mwanasiasa anaweza kuwa kiongozi mzuri sana, kwasababu msingi wa uongozi kidunia umewekwa katika siasa, na mwanasiasa hupenda kuongoza... Mwanaharakati aweza kuwa mwanasiasa, lakini mwanasiasa hawezi kuwa mwanaharakati baada ku graduate kuwa mwanasiasa... Mwanaharakakati anajengwa katika ukosozi kwa mwanasiasa.
Julius Kambarage Nyerere, katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Ukurasa wa 8, anasema hivi:
"Awali baadhi ya Viongozi wa Chama - walikuwa wameanza kampeni za kutaka Rais Mwinyi aongezewe vipindi vya muda wa kuwa Rais.
Nilipotambua hivyo nilikuwa nimekwenda mara moja kwa Rais na kumsihi azizime kampeni hizo; na viongozi wahusika nilitafuta nafasi nao nikawaomba wasilifufue jambo hili. Nikadhani tumeelewana hivyo.
Kwahiyo nilishtuka niliposikia kuwa kumbe suala hilo la vipindi vya urais bado linazungumzwa, na ati bado uamuzi wa vipindi vingapi haujafikiwa! Kwahiyo nilirudia tena kueleza umuhimu wa kukubali kwamba suala hili tumekwisha kuliamua, na hatari ya kuanza kulizungumza upya.
Sababu ya kufanya muda ambao mtu yeyote anaruhusiwa kuwa Rais utamkwe na uwe ni sehemu ya Katiba ilikuwa ni kuutoa uamuzi huo mikononi mwa Rais mwenyewe au kikundi cho chote cha Chama au Dola. Si uamuzi mwepesi, kwa Rais wala kwa washauri wake"
Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi maana wana sifa mbili muhimu: Kwanza wana uwezo wa kutawala, na pili hawapendi kutawala. kwa hiyo jamhuri ya plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikiisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda.
Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa plato; Watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala, hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kutawala...
Kwa Tanzania hasa watu walioupinzani wengi wao ni wanaharakati ndiomaana wengi wanapigania taifa na wanauchungu mkubwa na taifa, furaha yangu ni kuwa wengi wao wana graduate kwenda kwenye uanasiasa... Hii ni dalili njema kwamba upinzani sasa unaweza kushika dola na kuongoza nchi... Mh Mbowe, Mh Mashinji ni mifano ya graduate wazuri wa siasa... Chachu kubwa imekuja baada ya uchaguzi mkuu 2015 na ujio wa "Mwanasiasa" nguli Mh Edward Lowassa...
Lakini kwa uzoefu na utafiti wangu mdogo wa siasa za Afrika nivigumu kwa chama kilichomadarakani kutoka madarakani kwa njia ya siasa za karatasi, lazima harakati za kimapinduzi ziongoze oparesheni hiyo...
Hivyo kwakuwa ccm haitatoka kwa kura za karatasi, chadema inahitaji wanaharakati wa kisiasa wengi zaidi kuliko wanasiasa halisi ili wasaidie ku freeze udikteta na uimla wa chama tawala...wanaharakati ndio wanaoongoza maandamano na ghasia za kisiasa zinasaidia kuwatoa madarakani mumiani wa leo...
Na Yericko Nyerere