Hayo majjna ya majini ni majina ya koo zao sio majina ya jini mmoja mmoja. Yapo ya koo za Kiafrika (kama mzuka, kibwengo, makata, n.k.) lakini pia zipo koo za Kiarabu (kama Sharifu, Ruhani n.k.). Yapo ya koo za kizungu pia. Unaweza kumsikia Mwafrika ambaye hajawahi kwenda shule kabisa, akieleza kwa Kiingereza kizuri kabisa mambo fulani wakati ambapo amepandisha pepo. Pepo likiondoka, hajui hata neno moja la Kiingereza.