Majina ya kiarabu na kizungu ni ishara ya kumjua Mungu?

Nilufer

JF-Expert Member
May 10, 2012
9,566
13,540
Hivi mtu akitaka kumjua mungu lazima ajikite kutafuta majina ya kizungu kama ni mkristo au ya kiarabu kama ni muislamu?

Hivi tumetekwa akili kila sehemu kweli? Yaani mtu akijiita Mwamfupe na akajikita kusali na kumuomba Mungu sana bado unaonekana siyo mkristo halisi eti kusa haitwi John au Peter!
Ukitaka kumjua Alah eti lazima uitwe Abdulkadri badala ya mlope.

Hivi huyu Mungu kweli hatujui sisi waafrica kama tunastahili mpaka tupitie kwa wazungu au waarabu ndo tujione fahari!!!

Hata lugha kanisani na misikitini ni totally foreign kana kwamba Mungu anatuona sisi ni wapagani na manyani.

Naenda maparokiani utaona mapadre wameassimilate culture za magharibi mpaka namna ya kula. Ukila kwa mikono mitupu kwa mapadre unaweza fukuzwa na kuonekana shetani. Wao hula kwa kitumia vijiko hata kama ni ugali.

Turudi kwa waislamu mfano huyu shehe Mkuu wa Dar anajilazimisha hata namna ya kuongea ifanane na waarabu Kabisaaa.

Hivi kweli sisi mungu alitulaani kabisa.
Ndiyo mana mi saa zingine nawapongeza wachina kwa kutotukuza imani za kimagharibi wao wanazo za kwao hata wahindi.

Lazima tujikubali bwana aaa!!!!!!
 
Kwa kweli sisi waafrika ni wapumbavu kweli.wengine hata rafudhi wanaiga ya kkimagaribi kana kwamba hawakijui kiswahili wakati wa ibaada.
Kuna wengine ndio wapumbavi haswaaa unakuta anaimba kiarabu na kukalili swala utadhani Mungu hasikii kisukuma.
Yaani nilaana ya kiwango cha bitumen.
Mara mohamed mara majid mara Ally mara mansour. Mara leicister mara rodrick mara pacifique.duuh Twafwaaa
 
Kiukweli sisi miafrika ni mijinga sana na milimbukeni. Ukipata mtoto halafu waambie rafiki na ndugu zako wapendekeze jina utasikia: Camilla, gabrela, Brian, Catherine, nk. Unakuta mtoto blackiiiiiiiii halafu anapewa jina BIACA ambalo maana yake ni mweupe.
 
Tatizo Dini ilivyoletwa na Wamissionari ililetwa kama kilainishi cha kumtawalia mtu mweusi.
Yaani kukufanya ujione duni, Mzungu awe bora. Lakini imani katika misingi yote haiihitaji Uitwe jina la kizungu au Kiarabu ili uonekane Mkristo au Muislam Bora.

Huo ni Ushamba Tunaopaswa kuupinga na kuukemea.
 
kuna uzi wangu kule jamii intelligence nimedadavua jinsi yesu na biblia ni feki,ni uzushi wa wazungu walioutengeneza kutawala akili za weusi na race nyingine,na kama biblia ni feki,quran nayo ni walewale feki feki
Imani za dini zipo. Ukristo sio wa wazungu, Kwa imani unakutana nao hadi Kwa Mwanadamu wa Kwanza adam na hawa ambao hawamilikiwi na watu wa kabila wala rangi yoyote.
Hivyo basi kama mababu zetu waliamini ktk Kuabudu Miti Mikubwa Haina tofauti na Mkristo anaeamini katika Mungu asiyeonekana na kwamba ameumbwa na Mungu huyu ambaye Kwa imani hiyohiyo anaamini yuko responsible na kila kiumbe.

Tatizo linakuja tunapoacha tamaduni zetu bora za kuitana Majina Yetu na Kukimbilia Majina ya kikundi kidogo cha wanadamu wenzetu na tamaduni zao za majina. Jambo hili Halikubaliki...
 
ukristo wa yesu ulitungwa na wazungu,get this right to your head
 
Nikisikia mtu anasema eti anamjua Mungu, automatically najua huyo ni chizi tu.

Unamjuaje Mungu asiyekuwepo?
 
Nikisikia mtu anasema eti anamjua Mungu, automatically najua huyo ni chizi tu.

Unamjuaje Mungu asiyekuwepo?
mkuu Mambo ya imani ni Kuwa na hakika na vitu visivyoonekana na mambo yatarajiwayo. Hutakuwa ujakosea ukiona mtu wa Imani kama chizi maana mnajadili kitu katika mawimbi tofauti yasiyohusiana.
 
mkuu Mambo ya imani ni Kuwa na hakika na vitu visivyoonekana na mambo yatarajiwayo. Hutakuwa ujakosea ukiona mtu wa Imani kama chizi maana mnajadili kitu katika mawimbi tofauti yasiyohusiana.
Hiyo maana ya imani huwa mnarithishana tu, haitoki kwenye fikra zenu.

Je unaweza kuniambia ni kitu gani kinachopima validity ya imani? maana watu wengi wameng'ang'ania imani potofu na hawataki kusikia kama ni imani potofu.
 
Koma kumlinganisha Mungu na allah!.

Koma kulinganisha Ukristo na uislam.

Uislam ulilnganishe na uabudu mizimu au dini zingine lakini usithubutu kuulinganisha na Ukristo.

Ungelimjua Mungu japo kidogo, usingelea mada ya kishenzi namna hii. Maana ungelijua maana ya majina katika kutukuza na kumsifu Mungu. Ungelijua majina yanabeba nini katika maisha ya mtu.

Nenda kajifunze kwanza kumjua Mungu ndipo upate maarifa ya kumjadili. Kinyume cha pale unataka kujadili Jambo usilolikua ambapo unaonyesha namna gani ulivyo mpumbaveu!.
hakuna mada ya kishenzi apa labda we ndio mshenzi na tamaduni zako za kilabu sijui za kizungu!!??
 
Koma kumlinganisha Mungu na allah!.

Koma kulinganisha Ukristo na uislam.

Uislam ulilnganishe na uabudu mizimu au dini zingine lakini usithubutu kuulinganisha na Ukristo.

Ungelimjua Mungu japo kidogo, usingelea mada ya kishenzi namna hii. Maana ungelijua maana ya majina katika kutukuza na kumsifu Mungu. Ungelijua majina yanabeba nini katika maisha ya mtu.

Nenda kajifunze kwanza kumjua Mungu ndipo upate maarifa ya kumjadili. Kinyume cha pale unataka kujadili Jambo usilolikua ambapo unaonyesha namna gani ulivyo mpumbaveu!.
Kwa hiyo wewe hapa ndo unamjua Mungu, wafia dini mna kazi sana
 
Koma kumlinganisha Mungu na allah!.

Koma kulinganisha Ukristo na uislam.

Uislam ulilnganishe na uabudu mizimu au dini zingine lakini usithubutu kuulinganisha na Ukristo.

Ungelimjua Mungu japo kidogo, usingelea mada ya kishenzi namna hii. Maana ungelijua maana ya majina katika kutukuza na kumsifu Mungu. Ungelijua majina yanabeba nini katika maisha ya mtu.

Nenda kajifunze kwanza kumjua Mungu ndipo upate maarifa ya kumjadili. Kinyume cha pale unataka kujadili Jambo usilolikua ambapo unaonyesha namna gani ulivyo mpumbaveu!.
Poooooovu tu, kumbe hujaelewa hata kilichoongelewa pamoja na kwamba kimeandikwa ili usome taratibu na kwa uyakinifu. Mleta uzi hajalinganisha dini ya mtu. Fanya tafakuri ww
 
Kiukweli tumekuwa wendawazimu wa IMANI huu ndik ukweli usiopingika, leo hii unakuta mtu ni mkristo wa KKKT au ROMAN, anaamua kuingia PENTEKOTE au kuokoka cha ajabu ni kuwa huyu mtu ana jina lake la asili mfano, TUSAJIGWE cha kushangaza unaambiwa badili jina maana ya asili yameshikamana na maagano ya baba na bibi yako. Huu mm nauona wehu kabisa. Istoshe kabla ya hawa watu kutufunza Imani yao tulikuwa na dini zetu hata kama wakisema ni za kipagani kama walivyozoea kuziita wao, lkn ifahamike tu kuwa tulikuwa na dini na imani zetu ambazo zilitufanya tuwe comfortable kuliko sasa. Ila kosa kubwa ni pale tulipokubali kuacha imani zetu na kufuata imani za wengine hapa MIUNGU yetu ikaamya kuwa MONSTERS kwa kufanya different revenge. ni hayo tu
 
Hiyo maana ya imani huwa mnarithishana tu, haitoki kwenye fikra zenu.

Je unaweza kuniambia ni kitu gani kinachopima validity ya imani? maana watu wengi wameng'ang'ania imani potofu na hawataki kusikia kama ni imani potofu.
Tunaomba maana ya imani unayodhani ilipaswa kutoka kwenye fikra zetu.
FAITH-complete trust or confidence in someone or something.
Imani kuwa valid au invalid ni mtazamo wa yule anaemjadili mwenye imani Husika au Socially agreed moral Standard.
Hakuna Faithiometer ambayo ni valid kwa kila imani. Inaweza kuwa Valid kwa wanaoamini Uwepo wa Mungu kipimo hicho hicho kikawa Invalidi kwa wanaoamini Kutokuwepo kwa Mungu ingawa zote ni imani.
 
Back
Top Bottom