Majina mapya ya mitaa Dar

Ukuta hapo pesa kubwa imepigwa. inashangaza vipaumbele kuwa majina ya mitaa badala ya kuboresha miundombinu hasa ya majitaka na hasa huku kwetu sinza. ni aibu
 
Haya majina yangeendana na sehemu yenyewe. Kuna wazee wa sehemu majina yao ni umaarufu at least wangetumia hayo iwe rahisi hata kumuelekeza mtu. Sasa mtaa wa ludewa ndani ya dar?
 

wewe mkuu unayekaa mtaa wa IRINGA unaoanzia pale mwenge zahanati ..
opposite na kanisa la wasabato ni jirani yangu....mimi niko pale karibu na uwanja wa mpira.
 
Watu wameshapiga pesa wameondoka zao. Nyie piganeni tu.
 
Mm nakaa kwa mfuga mbwa...eti sasa wanapaita wiles street...hili jina wapi na wap..?? manzese na uzungu wapi wapi
 
Mnazungumzia barabara au mitaa? Nijuavyo mimi mitaa ni mamlaka inayofuatia chini ya Kata, na wala huwa haiwekewi vibao
 
Huku kwetu kuna kwa Komba street. Kwa ndevu street. Maduka mitatu. Njia panda ya goba. Matosa street. Shule ya msingi. Kwa mpare. Kwa Mushi. Mzazi street. Kwa Ndunguru. Kwa mhaya street. Kwa Osama. Machinjioni. Kwa mrema. Kwa kichwa yaani hadi raha na wewe ukisogea kidogo ukajenga sehemu mpya basi wa jamani jina lake linakuwa LA kitongoji lako linakuwa la mtaa. Karibuni sana.
 
Kwa mfuga mbwa wanapaita wiles ha ha ha hata haiji
 
Unajua mtaa unaweza kupewa jina lolote lile. Baada ya muda hiyo mitaa itazoeleka. Kikubwa jina lisijirudie.

Kingine ni kuwa Tanzania hatukuwa na ustaarabu wa kuwa na mitaa na hata majina ya mitaa. Ni hivi karibuni tu ndiyo angalau tumeanza tena kupima viwanja na baada ya watu kupiga kelele ndiyo mitaa imeanza kupewa majina.
 
kuna mitaa dzm kama Mtaa wa libya,nyarung'ombe kkoo,naomba kujua chanzo cha kupewa hayo majina
 
Jamani katika hizo barabara naomba tumkumbuke waziri mkuu wa sasa ndugu Pinda ambae siku hizi simuoni kwenye tiivii au magazeti tusije tukamsahau kiongozi huyu muadilifu asiyekua na kashfa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…