Chadema hawana serikali lakini wana uwezo mkubwa wa kusimamia fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato.Mfano mzuri ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jimbo linaongozwa na mbunge naMadiwani ni wa Chadema.Mwaka 2010 Halmashauri ilkuwa inakusanya sh bn1.7 kwa mwaka lakini baada ya Chadema kuchukua Halmashauri mapato yanakimbilia bn 5 na si vyanzo vipya bali ni vile vile ikiwa ni pamoja na kuziba mianya mingi ya ufujaji.Madiwani walikuta vibanda vya soko kuu vinalipiwa sh7,500 wakati mtu huyo huyo anakodishia kwa shs 150,000 mpaka 250,000.Sasa hivi wanalipa Halmashauri sh 150,000 kwa mwezi.Barabara zinakarabatiwa kwa wingi kutokana na mapato hayo.Mabadiliko yanaonekana bila ubishi.Utaona wazi kwamba mleta mada yu sahihi kabisa.