Majimbo ya CHADEMA na unafuu wa maisha

kilght

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
634
181
Ilikuwa anawaomba wabunge wa CCM kuwaboreshea maisha wapiga kura wao hasa waishio vijijini kuwa kuna wengine tangu kuzaliwa kwao hawafaham umeme.

Hii khali ni tofauti kwa upande wa CHADEMA majimbo yao yote wanayoyaongoza kuna unafuu wa maisha wanainchi wao wana umeme maji barabara nzuri nk.

Maneno haya yamesemwa na Silinde mbunge wa Mbozi.
 
Nassari Joshua,"Mh. waziri naishukuru serikali (inayoongozwa na chama cha mapinduzi) kwa kupeleka umeme katika vijiji 6 kati ya vijiji 10 vilivyokuwa katika mpango wa kupeleka umeme vijijini(REA)."
 
ilikuwa anawaomba wabunge wa ccm kuwaboleshea maisha wapiga kura wao hasa waishio vijijini kuwa kuna wengine tangu kuzaliwa kwao hawafaham umeme.hii khari ni tofauti kwa upande wa chadema majimbo yao yote wanayoyaongoza kuna unafuu wa maisha wanainchi wao wana umeme maji barabara nzuri nk maneno haya yamesemwa na silinde mb mbozi

wewe kweli unaishi kenya, chadema imetoa wapi hiyo serikali ya kuyafanya hayo?? serikali ya ccm ndio watendaji wakuu, na majimbo yanaendelezwa kwa kutimiza sera za serikali ya ccm, hali ndio inazidi kua mbaya tokea wabunge wa chadema walipoingia, mfano mzuri ni arusha ambako uchumi umeshuka mno kutokana na hofu ileyoletwa na vurugu za maandamano ya chadema, labda tuwasifuwabunge wa chadema kwa matusi, maandamano, kutoka nje bungeni, kupigana, kung'oa mic bungeni, imebakia kukojoa tu, ndio maendeleo tunayoyaona kutoka kwa wabunge wa chadema
 
Chadema hawana serikali lakini wana uwezo mkubwa wa kusimamia fedha za serikali ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato.Mfano mzuri ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.Jimbo linaongozwa na mbunge naMadiwani ni wa Chadema.Mwaka 2010 Halmashauri ilkuwa inakusanya sh bn1.7 kwa mwaka lakini baada ya Chadema kuchukua Halmashauri mapato yanakimbilia bn 5 na si vyanzo vipya bali ni vile vile ikiwa ni pamoja na kuziba mianya mingi ya ufujaji.Madiwani walikuta vibanda vya soko kuu vinalipiwa sh7,500 wakati mtu huyo huyo anakodishia kwa shs 150,000 mpaka 250,000.Sasa hivi wanalipa Halmashauri sh 150,000 kwa mwezi.Barabara zinakarabatiwa kwa wingi kutokana na mapato hayo.Mabadiliko yanaonekana bila ubishi.Utaona wazi kwamba mleta mada yu sahihi kabisa.
 
mapato yanaongezeka moshi kwa kua hakuna maandamano na vurugu, si ndio nyumbani kwahiyo hamuoni sababu ya kuharibu kwenu, mnaharibu majimbo ya wenzenu, mradi ndugu yenu anapokea mshahara bungeni hajali kama watoto wa wenzake wanakufa kwa vurugu na fujo zinazoanzishwa na chadema, shame on you chadema.
 
Stroke,kwa taarifa yako baraza la halmashauri ya Moshi lina Madiwani mchanganyiko kwa maana ya makabila.Sasa unapozungumzia maandamano na habari ya nyumbani sikuelewi vyema.Usituhamioshe nje ya mada tuangalie mafanikio ili wote tujifunze na kutoa huduma bora kwa wananchi wetu popote walipo kwani ni watanzania na wana wajibu wa kuhudumiwa kutokana na kodi zao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom