Majibu yaliyotolewa leo na CHADEMA, ni ushahidi tosha kuwa hela zimepigwa

Hela ilikuwa inakusanywa kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Leo hela haipo kabla hata ya uchaguzi mkuu. Hela imepigwa tuache upofu.
Kama imepigwa si ndiyo ushahidi utolewe. Mana kuna tofauti kati ya hela kupigwa na kutumika kwa matumizi mengine!!
 
Hahahahahah kwaio mwita kadanganya hahaha Mungu awabariki Ila huu uchafu mnashindwa kuusafisha wakat huu kabla ya kampen Basi mjue mmejinyea wenyewe kwenye kampen mtapigwa mabom Ayo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahah kwaio mwita kadanganya hahaha Mungu awabariki Ila huu uchafu mnashindwa kuusafisha wakat huu kabla ya kampen Basi mjue mmejinyea wenyewe kwenye kampen mtapigwa mabom Ayo
Kwani Waitara ni msahafu wa kweli za dunia ya siasa za Tanzania?

Mnapowachukua watu toka CHADEMA huwa mnadhani mmemaliza kazi, lakini ghafla mnagundua kuna kazi wanatakiwa kufanya, hapo ndipo hujifanya wana siri za CHADEMA!!
 
Kama imepigwa si ndiyo ushahidi utolewe. Mana kuna tofauti kati ya hela kupigwa na kutumika kwa matumizi mengine!!
Ushahidi ndio huo. Hela iliwekwa kwa lengo lakufanikisha uchaguzi 2020. Sasa haipo, unataka ushahidi gani tena? Km zilienda kwenye matumizi mengine naamini Kuna vikao walikaa km chama kubariki hayo, tunaomba rejea za vikao. Tunaingiaje kwenye uchaguzi bila pesa?
 
Ushahidi ndio huo.
Hapa ndipo ninapopishana na wengi wenu. Ushahidi ili uwe ushahidi kuna kanuni zake za kufuatwa. Hayo maneno ya tuhuma ya Waitara siyo ushahidi.

Ndiyo maana nasema kama hela ziliwekwa si hata wataje akaunti hizo hela ziliwekwa na watia sahihi walikuwa wakina nani na ni kwa nini waliidhisha hela hizo zitolewe!!??
 

Sasa wewe una akili za mtoto au mtu mzima?
 
Tumepigwa 1.5 trn polepole akaleta hesabu za mezani. Ila hamwezi hoji izo pesa za umma. Kutwa kuhoji pesa za cdma. Kwanye report ya CIG CDM imepata hati chafu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie CCM acheni Longolongo. Mahesabu ya CHADEMA yalifanyiwa ukaguzi na CAG na kama kungekuwa na upigji CAG angesema. Kwa kuwa hajasema yote mnayoongea hapa ni porojo tu
 
Majibu siyo ushahidi wa wizi bali viambatanisho!! Mnaosema hela zimepigwa si angalau mtaje hata Akaunti moja iliyotolewa hela na ni nani aliyeidhinisha kutolewa kwa hizo hela!!
Ccm wamezoea utapeli na ulaghai

Wanadhani watanzania wa 2020 ni sawa na wale wa 1995 kiasi cha kuwadanganya kirahisi rahisi tu
 

Kulalamika ni kawaida tu
Hata mke wako au dem wako ukimuacha leo no wonder akalalamika kuwa ulikuwa haumridhishi kitandani so ni jambo la kawaida tu
 
Chadema hawatakiwi kutoa majibu,wakitoa majibu watakua wanajipendelea,majibu yanatakiwa yatolewe na hao hao serikali.

Na funny enough,serikali hiyo hiyo ilishatoa majibu kupigia CAG kwa kutoa na hati maalumu kabisa!

Inaitwa hati ya ukaguzi na ni SAFI!

Hilo ndio emperical answer lisilokua na makandokando!
 
Mkuu Allen Kilewella, utaendeleza ubishi usio na faida kwa chama chako. Na wala sina haja ya kuendeleza mjadala na mtu asiyekubali ukweli.

Walioanzisha tuhuma dhidi ya Mbowe ni viongozi wa CHADEMA waliokihama na wanaohama (sihitaji kuwataja majina maana unawajua). Kumshutumu Waitara ni moja ya sababu ya kuwaambia mnahamisha goli.

Bado nasisitiza, wagombea wa CHADEMA watakuwa na mtihani mgumu kumsafisha Mbowe na genge la viongozi wenzake, katika kampeni za Uchaguzi Mkuu, 2020, iwapo MWAMBA atatoa ruhusa ya kushiriki. Ukweli ni kwamba kuna kapu, kama siyo gunia, la tuhuma dhidi yao.

Ni wajibu wako, na wenzako humu JF na mitandao ya kijamii, kutoa ukweli/uwongo wa tuhuma hizo badala ya kuendeleza lawama kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa CCM.

Lijuakali alihitimisha tuhuma dhidi ya Mbowe, MWAMBA wenu, akinukuu ukweli wa kisayansi kuwa "kwa kila kitendo kuna tendo sawa la kinyume" au kwa lugha ya kigeni "For every action, there is an equal and opposite reaction" (Newton's Third Law of Motion). Nisingependa kutumia msemo wenu, mnapokosa hoja, kuwa WAKATI NDIO JIBU, lakini ukweli ni kwamba tuhuma hizo zitakigharimu chama.

Haiwezekani na haingii akilini mwa watu wazima, ati viongozi wanaokihama chama wananunuliwa kama bidhaa. Hayo ni matusi ya nguoni. Wanaodai hivyo wanajidharilisha na nafsi zao zinawasuta. Ina maana CHADEMA hua inanua viongozi, basi wataje bei ya kununulia.

Hoja nyingine ya USALITI kwa viongozi wanaohama CHADEMA siyo tu ni ya kupuuzwa, ni ya kinafiki. Je, wale wanaohamia CHADEMA, waitweje? Kama vyama wanakohama pia watawaita "wasaliti", ni dhahiri CHADEMA kimejaa viongozi wasaliti, hivyo basi kinakosa uhalali wa kupewa madaraka kuongoza nchi hii.
 
Kwa upande wangu, tukisimama kwenye hoja haiwezekani tuhuma zikatolewa na upande mmoja halafu tukatoa hukumu na bado tukajiona ni sisi ni 'great thinkers'. It's a joke! Kitu kingine, morally, kama hakuna ushahidi siyo ushahidi kuwa mtu hakula hela na wala siyo ushahidi kuwa mtu kala hela. Lakini kwa utaratibu wa kisheria tunazozifuata na kuzitumia, anayetuhumu ndiye anayepaswa kuthibitisha tuhuma zake. Mfano, A akisema B ni mwizi, basi A anapaswa athibitishe kuwa B ni mwizi. Vinginevyo, inakuwa tu 'vicious calumny' ambayo kama Watanzania inabidi tuepuke na tuondokane nayo na kama hatuwezi, itakuwa ndiyo tabia yetu. Maana leo tufanya hivyo kwa X, kesho kwa Y, keshokutwa kwa Z na tutaendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…