By Salma Said, Mwananchi
Zanzibar. Wakati Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikijiandaa na uchaguzi wa marejeo kumetokea sintofahamu za kisheria juu ya fedha zitakazotumika katika uchaguzi huo kukosa ridhaa ya Baraza la Wawakilishi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wanaharakati wamesema haiwezekani fedha za Serikali kutumika bila ya kuidhinishwa na Baraza hilo kwa kuwa lilikwishavunjwa.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohammed Aboud alisema:
“Sikiliza, nchi haiwezi kuendelea kukaa hivi bila ya uchaguzi, lazima ufanyike Baraza la Wawakilishi liwepo au lisiwepo.”
Alipotakiwa kueleza fedha hizo zitatolewaje bila ridhaa ya Baraza la Wawakilishi, alisisitiza: “Uchaguzi utafanyika tu na wenye jukumu la kutangaza siku ya uchaguzi ni Tume ya Uchaguzi Zanzibar, kwa hivyo wacha watangaze siku kisha tuone. Uchaguzi ni lazima nchi haiwezi kuwa hivi.”
Hivi karibuni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake Vuga kuwa; “bajeti ya uchaguzi imeshapatikana na kinachosubiriwa ni Tume ya Uchaguzi Zanzibar kupanga siku ya uchaguzi tu.”
Akizungumzia hali hiyo, mwanasheria Khalled Said Gwiji alisema: “Nchi yetu inaongozwa kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko wa taaluma na uelewa. Viongozi wetu wengi wa kisiasa wanapishana na uelewa wa wataalamu.”
Alisema kifungu cha 88 (c) na (d) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza kazi za Baraza ikiwamo kuidhinisha na kusimamia mipango ya maendeleo ya Serikali katika njia ileile ambayo Bajeti ya mwaka inaidhinishwa.
“Nani anayeiuliza Serikali? Nani anayeidhinisha mipango ya maendeleo ya Serikali? Kama hakuna, wanaoyafanya hayo watambue kuwa wanavunja Katiba.”
Ali Hamad Mafadhiy, kutoka Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha Zanzibar, alisema haamini kama Serikali ina fedha ilizotenga kwa ajili ya uchaguzi na kama zipo, alishauri zitumike katika masuala mengine.
Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), Omar Said Shaaban alisema Katiba ya Zanzibar 108 (1) inasema Baraza la Wawakilishi linaweza kutunga sheria kuanzisha mfuko wa matumizi ya dharura na kumruhusu waziri anayeshughulikia mambo ya fedha kutumia mfuko huo iwapo ameridhika kwamba ni jambo la dharura na la muhimu.
Alisema hicho ndicho kifungu kinachoweza kutumika lakini inategemea kuwapo kwa sheria inayoweka utaratibu wa kufanya matumizi ya dharura. “Kifungu chenyewe kinaweka mazingira hayo, lakini swali la kujiuliza je, sheria yenyewe ipo?”