MAJI yatangazwe dharura ya Taifa

Mzee23

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
1,742
Reaction score
3,673
Habari wana jF!

Jambo moja ni hakika, MAJI ndilo hitaji kubwa zaidi la wananchi wanaoitwa 'wanyonge' hasa wa vijijini baada ya mazao ya Chakula. Nimeishi kijijini nimeshuhudia hili. Wakati wa Kiangazi ni mateso yasiyoelezeka! Kukesha kwenye chemchemi za maji, kwenda umbali mrefu hata kijiji cha sita kutafuta maji! N.k n.k

Kwa miongo mingi,toka uhuru hadi leo hadithi za wanasiasa wetu ni zilezile, awamu hii watasema ufinyu wa bajeti, awamu nyingine watawalaumu wazabuni wa miundombinu ya maji vijijini na awamu nyingine itasema upembuzi yakinifu umekamilika n.k n.k huku 'wanyonge' wakiendelea kutaabika!

Maoni

Kutokana na umuhimu na unyeti wa MAJI, Uchaguliwe mwaka mmoja wa fedha ambao Taifa litatangaza ukosefu wa maji kuwa hali ya dharura(National emergency) ambapo bajeti nzima ya maendeleo ya mwaka huo itaelekezwa kwenye maji.
Kwamba ibaki tu pesa ya kulipia mishahara ya watumishi na dharura zingine huku pesa za maendeleo za wizara zingine zote ipewe wizara ya maji, mipango mingine yote isimame.

Hizi trilioni zitakazopatikana, penye uwezekano wa kuvutwa maji toka vyanzo vikuu kama maziwa, yavutwe, penye maji ardhi visima vichimbwe n.k lengo kuhakikisha kila mita 100 toka kaya ina maji.

Barabara za rami,changarawe, umeme vinavyohangaikiwa na watawala sasa ni ANASA kwa wananchi 'wanyonge' wa vijijini. Wao wakipata MAJI huku mazao yao ya chakula yamekubali basi.
 
Dharura ya serikali hii ni chadema, wewe sema tu kisima cha maji kimejengwa na chadema maeneo ya nkuhungu aisee kesho yake utakuta nkuhungu nzima ina maji ya kutosha
 
Dharura ya serikali hii ni chadema, wewe sema tu kisima cha maji kimejengwa na chadema maeneo ya nkuhungu aisee kesho yake utakuta nkuhungu nzima ina maji ya kutosha
Niliwahi kuliona hilo pia ktk siasa zetu!

Wewe ni mkaazi wa Nkuhungu chama,kanisani au kwa swai mkuu!
 
Waweke mkakati wa kuvuna mvua. Mafuriko kila sehemu Huku wengine wanadai hawana maji!
 
Waweke mkakati wa kuvuna mvua. Mafuriko kila sehemu Huku wengine wanadai hawana maji!
Yaani mkuu mikakati ipo kitambo ya kinachotakiwa kufanywa lakini siku zote hulaumiwa bajeti finyu! Mfano Dar.. Baada ya mafuriko Jangwani hapa majuzi tukamsikia Mkuu wa mkoa anadai mpango wa kuvuna maji upo! Lini sasa utekelezaji?

Ndio maana naona itangazwe dharura ili kila mkakati ugeuzwe kitu halisi!
 
Reactions: Auz
Maajabu Ya Karne ! Kuna Kijiji Kimoja Mkoani Singida Wilayani Manyoni, Halmashauri Ya Itigi Kata Ya Aghondi Kinaitwa Njirii Mpaka Sasa Wananchi Hawana Maji Safi Ya Bomba.

Wanatumia Maji Ya Madimbwi Ambayo Si Salama Kutokana Na Uwezokano Wa Kutumiwa Na Wanyama Wa Porini Na Wa Nyumbani.

Kijiji Kinapitiwa Na Barabara Kuu Ya Lami Mwanza - Dar Na Kimepata Umeme Wa Tanesco Lakini Hakina Mabomba Ya Maji Wala Mradi Wowote Wa Maji Safi, Wananchi Wanakunywa Maji Yenye Tope.

Inashangaza Mbunge Na Diwani Wa Eneo Hilo Wanafanya Kazi Gani Kuhakikisha Wananchi Wanakunywa Maji Salama?

Miradi Ya Maji Vijijini Ni Kitu Kinachowezekana Kama Viongozi Ni Wabunifu.

Kuna Umeme Wa Jua Na Upepo Kuweza Kutumika Kama Nishati Kuendesha Mitambo Ya Kuvuta Maji.

Viongozi Wabunifu Ndiyo Wanayoleta Maendeleo Ya Wananchi
 
Mara zote huwa nasema viongozi wa nchi hii wana Laana. Tuna Maziwa, Mabwawa, Mito na Bahari ila maji ni changamoto. Ila magari ya milion 200 kununua wala sio shida!
 
Mara zote huwa nasema viongozi wa nchi hii wana Laana. Tuna Maziwa, Mabwawa, Mito na Bahari ila maji ni changamoto. Ila magari ya milion 200 kununua wala sio shida!
Tunaongoza mkuu ktk ukanda huu kwa vyanzo vingi vya maji(water bodies) sijui nani azaliwe/afufuke/ashuke awastue viongozi wetu mahitaji halisi ya watu!
 
Tunaongoza mkuu ktk ukanda huu kwa vyanzo vingi vya maji(water bodies) sijui nani azaliwe/afufuke/ashuke awastue viongozi wetu mahitaji halisi ya watu!
Saudia sehemu kubwa ni Jangwa lakini wakazi wa pale hakuna anaeijua adha ya maji wala umeme. Mwanza hapo kuna ziwa Nyanza na mabwawa kadhaa lakini kuna vijiji vina shida ya maji hujawahi kuona wakati ziwa lipo takriban km 10 tu au tano ila wanaishia kwenda kutafuta mboga tu
 
Mkuu unaijua vizuri saudia yote? na umewahi kutembelea vijiji vya ndani ndani kabisa? au saudia unayozungumzia wewe ni mijini tu unakoendaga?
 
Cha kushangaza maji wala hayatajwi kama kipaombele !

Karibia miaka 60 ya uhuru lakini bado maji ni mtihani mkubwa sana kama huduma ya msingi kwa binadamu!
 
Cha kushangaza maji wala hayatajwi kama kipaombele !

Karibia miaka 60 ya uhuru lakini bado maji ni mtihani mkubwa sana kama huduma ya msingi kwa binadamu!
Siku ukibahatika kumwona waziri wa maji amewekwa kikaangoni bungeni kuhusu maji utamwonea huruma! Bajeti kiduchu na itakayotolewa kwa matumizi ya wizara ni kiduchu zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…