singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema watumishi wa umma wako huru kuhamia kokote wapendako, lakini wahakikishe wanaenda huko wakiwa safi na kamwe mtu asiharibu kazi akitarajia kuwa atahamishiwa sehemu nyingine.
“Serikali hii haina utumishi kwa mtu aliyeharibu kazi. Usije ukaharibu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda kuendelea na kazi. Serikali ya awamu hii haina nafasi na watumishi wa aina hiyo,” alisema.
Waziri Mkuu alisema hayo akiwa wilayani Itilima jana ambapo alifafanua pia kuwa mtumishi mchafu watamalizana naye papo hapo: “Tutamalizana naye na shughuli yake itakuwa imeishia hapo,” na kwamba huo ndio utaratibu wa Serikali ya Awamu ya Tano. Aidha Waziri Mkuu aliongeza: “Serikali hii haitawafumbia macho watumishi wasio waadilifu, waaminifu na wasiowajibika. Hatutahamisha mtumishi mzembe kutoka Bariadi kwenda Bunda, tutamfukuza kazi… hatutamwonea mtu yeyote, msiwe na hofu, mwenye hofu ni yule mwenye matatizo.”
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo jana wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Itilima kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambao ameuzindua jana wilayani Itilima, mkoani Simiyu.
“Watumishi wenzangu huu ni wakati wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya Awamu ya Tano ukoje. Jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi wala dini zao,” alisisitiza.
Waziri Mkuu aliwahakikishia watumishi hao kwamba Serikali inatambua changamoto walizonazo kutokana na upya wa wilaya hiyo na mkoa huo na akawaahidi kuwa ataboresha mazingira yao na hawana sababu ya kuwaadhibu wananchi kwa utumishi dhaifu na kuwadai rushwa kwa madeni wanayoidai serikali.
“Msiwaadhibu wananchi kwa kisingizio cha mazingira magumu ya kazi zenu, tunajua mnayo madai ya nauli, posho za mafunzo, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya likizo,” alisema huku akishangiliwa na kuongeza kuwa serikali itayalipa madeni hayo japo haitamaliza yote kwa wakati mmoja, ila ana uhakika wa kukamilisha walau kwa asilimia 80.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kusimamia watumishi wa umma ili watende kazi zao kwa ufanisi na kuleta tija kwa Taifa na kwamba serikali yao haina uhamisho wa mfanyakazi mchafu.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika mkakati huo wa kuhakikisha watumishi ‘wachafu’ wanaadhibiwa, jana alisema amemfukuza kazi muuguzi aliyefanya uzembe na kusababisha mjamzito kupoteza pacha katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba wengine watano watafunguliwa mashtaka ya mauaji.
Waziri Mkuu alisema serikali haitasita kuchukua hatua kama hizo kwa mtumishi yeyote yule atakayeshindwa kuwajibika. Alirejea kauli yake kuwa serikali inatambua inadaiwa na watumishi wa umma na inafanya jitihada za kumaliza malimbikizo ya madeni hayo na pia kuweka mifumo ambayo haitazalisha tena malimbikizo.
“Tuna uhakika tutafanikiwa kumaliza malimbikizo hayo na hasa wakati huu ambao makusanyo ni mazuri. Msikiuke miiko ya utumishi eti kwa sababu unaidai serikali…hasira hasara,” alisema Waziri Mkuu. Kuhusu usimamizi, aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanasimamia utendaji.