Maiti ya Mwanamke mwenye waume wawili yazua utata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti ya Mwanamke mwenye waume wawili yazua utata

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Feb 18, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utata huo ulizuka jana maeneo ya Tandale Magharibi, baada ya wanaume wawili mmoja aitwae Abdul na mwingine Salum kugombania maiti ya mwanamke mmoja aitwae Tausi Hassan [36] kila mmoja akidai alikuwa mkewe wa ndoa akitaka kwenda kuuzika.

  Zogo hilo lilizuka baada ya Tausi pamoja na mwanae aitwae Faim Salum kufariki dunia baada ya marehemu na mwanae wakiwa kwenye bajaji kugongwa na gari la taka eneo la Magomeni Mapipa.

  Inadaiwa na ndugu wa karibu wa mume wa kwanza wa marehemu kuwa, wakiwa nyumbani kwa mume wa marehemu wakijitayarisha na taratibu za mazishi walijitokeza wanawake wapatao watano wenye asili ya kiarabu wakidai wapewe miili yote miwili Tausi na mwanae waende kuizika.

  Katika kitu ambacho hakuna mtu ambaye alitegemea mahali pale wakinamama hao walitoa cheti cha ndoa kinachoonyesha Abduli na Tausi walifunga ndoa huko Kariakoo Mtaa wa Jangwani jijini Dar es salaam.

  Baada ya zogo kubwa kuzuka ndugu wa marehemu waliamua kuuchukua mwili huo na kwenda kuzika kijijini kwao Tungi Mkoani Morogoro.

  Inadaiwa kuwa marehemu alifunga ndoa na wanaume wawili bila mume wake wa kwanza kutambua hilo.

  Inadaiwa kuwa kwa mara ya kwanza marehemu alifunga ndoa na Salum Senela mwaka 1998.

  Pia mwanzoni mwa mwaka jana marehemu ilidaiwa kafunga tena ndoa na Abdul hapahapa jijini Dar e salaam.

  Inadaiwa marehemu alikuwa anaweza kuzimiliki ndoa hizo mbili bila wasiwasi na alikuwa anawapa zamu wanaume hao bila kutambua kinachoendelea.

  Jamii na ndugu zake marehemu wamesikitishwa sana na tukio hilo kwa kuwa walikuwa hawafahamu kama alikuwa na waume wawili na ajali hiyo ya gari ndio iliyosababisha yajulikane yote hayo.

  Source: Nifahamishe.com
   
 2. B

  Babuji Senior Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii kali si mchezo
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  RIP Tausi na Mwanao ......but maisha yako duniani were terrible! Mi si hakimu, Mungu atatoa hukumu yake kwa maisha yako ya duniani! Amen
   
 4. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Du Du Du ukishagaa ya Musa utaona ya Firauni. Haya mambo makubwa inaelekea ni fundisho kwa sisi tuliobaki duniani kuhusu mahusiano haya na mienendo yetu kwa ujumla.
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na kama hili limekuwepo basi mengi ya aina hii yapo kuweni macho.

  Mungu atusamehe kwa maovu yetu hapa duniani.

  Tausi sidhani kama alipata muda wa kutubu kwani si alikufa kwa ajali?- ni fundisho kwetu kuwa kifo tunatembea nacho tujiandae muda wote tuepuka kuwatendea maovu wenzetu kwani tunaweza tusipata nafasi ya kuwaomba msamaha.
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  alikuwa anaagaje kwa mume 1 kwenda kumuhudumia mume mwingine?haaakazi kweli! RIP.
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hiyo pia kali, duh
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hii ndiyo haki sawa inayodaiwa na wanawake.Mbona wanaume ,tena kwa siri, wanakuwa na nyumba ndogo?
   
Loading...