Maisha yanafurahisha Sana

Maisha yanafurahisha Sana

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,101
Wakati wewe unapanga kutoka kigoma ili uhamie Dar es salaam kuna mtu na yeye anapanga kuishi Kigoma, wakati wewe Unapanga kuacha biashara ya Daladala mwenzako anapanga usiku na mchana kuanza biashara ya Daladala, wakati wewe una ndoto ya kwenda Ulaya kuna wengine wana ndoto yakuja Africa.

Maisha ni kama mchezo wakubadilishana vitiji,yaani mfano umeona biashara ya Daladala ni ngumu na unataka kuacha ni Lazima utauza Gari kwahiyo unapouza gari ni kwamba umemuingiza mtu mwingine baada ya kutoka wewe,ndio maana mtu anajiuliza kama biashara fulani ni ngumu mbona watu wanaendelea kufanya?

Ukweli ni kwamba kabla mtu ajatoka kwenye biashara fulani anaweza kumuingiza mtu mwingine kwa namna moja au nyingine..
 
Back
Top Bottom