boyson onlye
JF-Expert Member
- Sep 13, 2015
- 1,108
- 1,404
Kufikiri wenye pesa wote wana akili zaidi kuliko wewe ni kujiumiza bure tu.Nawasalimu
Kuna ile Hasira iliyoko ndani yangu ya mafanikio kuna yale mawazo yaliyoko katika ubongo wangu wa namna ya kupata mafanikio, kila nikijaribu nafanikiwaje sioni njia, unakata tamaa asubuhi unajipa moyo labda leo itakuwa siku ya furaha, lakini wapi ukipita barabara unajiuliza mtu amewezaje kupata pesa mpaka akanunua pikipiki mwingine amewezaje kupata pesa mpaka akanunua gari na huyu anapataje pesa ya kujenga unakaa unafikiria inakatisha tamaa
Unadaiwa na watu wako wote wa karibu unaona kabisa upendo wa ndugu umepungua unajihisi wewe ni binadamu usiye na akili duniani maana unashindwa kufikiria njia ya kupata pesa kama wengine wanavyopata, unaishi mwenyewe hakuna kijana mtu wa makamo hata Mzee wa kukutia moyo na kukushauri, unajihisi mpweke dunia imekuelemea, ukienda kwenye Nyumba za ibada unaona wenzako wanaenda kutoa sadaka wewe unashindwa hata kunyanyuka, unaona namna ambavyo wana ahidi michango mikubwa na mafungu ya kumi ni mamilioni ila unashindwa kutoa elfu moja maisha yanachosha
Washikaji wanashindwa kukuonyesha hata njia au kukupa madili unaachwa na mchumba kisa unaonekana huna future (angejua yaliko kichwani) hakika asingewaza hayo yote
Maisha yanachosha umejitahidi kusoma na mpaka sasa yule uliyemzidi elimu amepata mpenyo wa pesa ila ww huna chochote cha kuuza ukiwa na shida, Maswali kichwani hayaishi nifanye nini, nipataje pesa, nitakuwaje tajiri, nitaishi hivi mpaka lini? Nitakuja kuwa na familia siku moja itaishije kama Hali yenyewe ndio hii
Akili imechoka moyo umeondoa tumaini mbili huna nguvu, unatamani kuzima simu maana ukipigiwa simu ni mtu anakumbusha Deni lake,
Maisha yanachosha
Hapa tusiwe ma "motivational speakers", hiko ulichoandika asimilia kubwa ya vijana tumepitia,tutapitia na tunapitia
Na hapo ulipo huwezi kujitoa wewe mwenyewe,ni UONGO
Hii ni siri niliyoanza kujifunza,unahitaji pesa,sawa?
Hakuna anayeweza kukupa pesa yake bure,eti kwa kumuelezea tu matatizo yako,probability ya watu kama hao ni almost zero
Hivi umeshawahi kujiuliza watu wanatoaje pesa?
Wape kitu kinachoongeza "value" kwenye maisha yao,njoo na bidhaa au idea yenye uwezo wa kutengeneza value kwenye maisha yao
Assume una Tsh 0.00,ila una ubongo
Fikiria kitu gani ukinambia Mimi kwenye Tsh 5,000 mkononi kitanifanya nikupe Tsh 1,000 yangu
Njoo na wazo au kitu kitakacho nipa mimi mwenye Tsh 5,000 value ya Tsh 3,000 halafu niuzie hiko kitu au hilo wazo kwa Tsh 2,000
Hapo tutakua tumetengeneza Tsh 1,000 out of nothing, na kesho nitawambia wezangu wenye Tsh 5,000 na zaidi kuhusu wewe
Huna pesa,usilalamike na kukataa tamaa,hii dunia haina huruma
Ndio maana hata binadam alitengeneza "After Life" kwa ajiri yake tu,ushawahi jiuliza "Sokwe" wakifa wanaenda wapi?
Jifunze kutengeneza pesa out of nothing, jifunze kutengeneza kitu chenye "value"
Jifunze valuable skills,kuwa best kwenye hio skill
Watu watakupa pesa tu
Unaweza kujifunza jinsi gani ya kutengeneza idea itakayo tengeneza thamani/valueNdo umpe sasa ideas za kutengeneza pesa out of nothing..maana hapo tatizo ndo lilipo
Hapa tusiwe ma "motivational speakers", hiko ulichoandika asimilia kubwa ya vijana tumepitia,tutapitia na tunapitia
Na hapo ulipo huwezi kujitoa wewe mwenyewe,ni UONGO
Hii ni siri niliyoanza kujifunza,unahitaji pesa,sawa?
Hakuna anayeweza kukupa pesa yake bure,eti kwa kumuelezea tu matatizo yako,probability ya watu kama hao ni almost zero
Hivi umeshawahi kujiuliza watu wanatoaje pesa?
Wape kitu kinachoongeza "value" kwenye maisha yao,njoo na bidhaa au idea yenye uwezo wa kutengeneza value kwenye maisha yao
Assume una Tsh 0.00,ila una ubongo
Fikiria kitu gani ukinambia Mimi kwenye Tsh 5,000 mkononi kitanifanya nikupe Tsh 1,000 yangu
Njoo na wazo au kitu kitakacho nipa mimi mwenye Tsh 5,000 value ya Tsh 3,000 halafu niuzie hiko kitu au hilo wazo kwa Tsh 2,000
Hapo tutakua tumetengeneza Tsh 1,000 out of nothing, na kesho nitawambia wezangu wenye Tsh 5,000 na zaidi kuhusu wewe
Huna pesa,usilalamike na kukataa tamaa,hii dunia haina huruma
Ndio maana hata binadam alitengeneza "After Life" kwa ajiri yake tu,ushawahi jiuliza "Sokwe" wakifa wanaenda wapi?
Jifunze kutengeneza pesa out of nothing, jifunze kutengeneza kitu chenye "value"
Jifunze valuable skills,kuwa best kwenye hio skill
Watu watakupa pesa tu
Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.Unaweza kujifunza jinsi gani ya kutengeneza idea itakayo tengeneza thamani/value
Ila sio kupewa tu hizo idea,
Atazame wapi kuna malalamiko,hapo ndipo kuna fursa
Halafu aje na jawabu lake kuhusu namna ambayo anaweza kutumia fursa iliyopo kwa kuondoa hayo malalamiko
Hilo jawabu au idea atakayo kuja nayo ndiyo itakayo mpa pesa kwa kuwa imetatua malalamiko yaliyopo na kuweka value kwa walalamikaji
Kama hilo jawabu lipo ndani ya skill alizonazo ni vyema,kama linahitaji skill mpya ajifunze au atafute wenye hizo skills
Kama jawabu lake linahitaji pesa ili likamilike,atoke kwenye "comfort zone" yake na kutafuta watu atakao washawishi kufadhili jawabu au idea yake as long as watafaidika
Ni hivyo
Umeongea point ya msingi sana. Mtoa mada anatakiwa kuacha kuangalia maisha ya wengine! Kila mtu ana siri ya mafanikio yake. Unaweza ukamuona mtu anaendesha gari, kumbe ni la mkopo tu!!Life isn't fair.
Acha kuangalia wengine na acha kujifananisha nao au subiri kufa kwa stress.
Kila mtu kazaliwa peke yake na atapita njia yake na atazikwa peke yake.
Hatua ya kwanza anza na kufuta Instagram kwenye phone yako.
NB: au utakufa kwa stress.