Maisha ya Mwanadamu, 9th February 2011 R.I.P Baba Mkubwa..tulikupenda!

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
maisha ya mwanadamu, kweli ni kama maua
lachanua tena li hamu, kesho lanyaukia
lapendeza tena li tamu, jua kuchwa mepotea
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

nashindwa kuvumilia, kulia japo kwa kimya
juzi tu tuliongea, leo hufungui taya
siku moja meugua, katutoka bila haya
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

ucheshi wako jamani, ujapo kutusalimu
na hadithi za zamani, zisofikia hatamu
kuondoka sitamani, ungebaki humuhumu
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

Sitosahau milele, nyimbo uzotuimbia
si kwa gita na kengele, tunzi ulizipangia
tena zilikuwa tele, kwa sauti kuvutia
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

kazi yake Mola, kamwe haina makosa
basi pema wewe lala, ila jua twakukosa
nasi tunafanya sala, Mbinguni sijekukosa
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

Metuachia simanzi, na giza la utotoro
pengo lako hata banzi, halizibi uchochoro
zimebaki zako kazi, t'tazienzi hata morrow
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

Kwaheri baba mkubwa, wajua tulikupenda
huzuni yetu ni kubwa, ila Mungu ndo kapenda
mipango yake mikubwa, tumebaki tunakonda
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

Umetutoka mapema, ulikuwa nazo nguvu
menifunza mengi mema, kutokuwa na uvivu
ukanifunza kusema, lugha mama bila wivu
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

siwezi kusema yote, ulonitendea hasa
tamaliza wino wote, ulijua na siasa
kikuyu na lugha zote, ulizifahamu hasa
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!

kwaheri umetutoka, baba mkubwa waona
machozi yananitoka, kuona nashindwa tena
na mahali hapa natoka, nguvu mie sina tena
kwaheri baba mkubwa, umetutoka mapema!
 
Kwakweli maisha ya mwanadamu siriye anayo muumba,mambo mengi tunayafanya na kuplan lakini Mungu kumbe ana lake juu ya mwanadamu huyu, japo mchakato wa maisha upo tight lakini popote ulipo hata kwa moyoni jitahidi kumkumbuka Muumba wako:A S thumbs_down:
 
Pole sana mshahiri hiyo ndiyo kazi ya mungu haina makosa cha kufanya tumuombee dua ili tutakapo fika peponi tukutane katika maisha ya raha mustarehee
amina
 
Back
Top Bottom