Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
MAISHA YA MASHAKA
Maisha yanakuwa mazuri kama utayaishi kwa viwango vyako mwenyewe.
Kama utaamua kuishi maisha yako kwa viwango vya wengine, maisha yako yanakuwa ya hovyo na yanakuwa maisha ya mashaka.
Njia moja ambayo wengi wanatumia kuishi maisha yao kwa viwango vya wengine ni kujilinganisha na wengine.
Na unapojilinganisha unakuwa kati kati. Juu yako kunakuwa na watu ambao unaona wamekuzidi kwa vile wanavyofanya au vile walivyo.
Chini yako kunakuwa na watu ambao unaona umewazidi kwa vile unavyofanya au vile ulivyo.
Kama mambo yangekuwa yanaishia hapa bado maisha yangekuwa bora sana. Ila sasa hayaishii hapa. Maisha yanazidi kuwa ya mashaka kutokana na watu hao wawili, watu hao wanakupa hofu kubwa sana.
Walioko juu yako wanakupa hofu kwamba wanapata zaidi yako au huenda wanaweza kukuzuia wewe usipate, au unaweza kuona wana mbinu za kukuacha wewe mbali zaidi. Hivyo unawahofia.
Walioko chini yako wanakupa hofu kwasababu unaona nao wanakazana ili kukupita wewe. Unaona kama ukizubaa kidogo basi watakupita na kukuacha nyuma. Hili linakupa hofu kubwa sana.
Kwa kujilinganisha na wengine maisha yako yanakuwa ya hofu na mashaka makubwa. Kila mara unafikiria kuna mtu anakuzidi au kukupita, ni maisha ya hovyo sana haya.