Maisha ya advance tabu

Ha ha ha nenda kwa majirani zako Tabora Boys ukawaulize wanatumia uchawi gani hadi wanatusua fresh
 
Nyau Wewe
Sxul ndo nini?

Hawa ndo wale wa kubadilisha mahala pa S wanaweka X
E.g
Mtumishi> Mtumixhi
Sasa> Xaxa

Pumbafu kabisa...

anyway we wa Advance Masomo ya hio combination unayosoma je una msingi mzuri??Unayamudu vilivyo??Hayo ni mambo ya msingi ambayo ulipaswa kujiuliza kabla ya kuanza kusoma!!
Milambo naifahamu ni shule ya serikali Changamoto nazifahamu mf. Ukosefu wa waalimu hasa katika masomo yako...
misosi duni..
Mi nimesoma bweni (nsumba boys) pia katika shule za sekondari so naelewa mambo yalivyo..ningependa nikusihi tu Ondoa dhana ya Ugumu katika masomo hayo..pia jitume kusoma kwa bidii,,fanya sana group discussions ndo siri ya mafanikio huko ulipo,,Likizo jiimarishe kwenye Tuitions soma piga topics na uzielewe Mwisho wa Siku Mungu atakujalia utapasua...Jitume mtoto wa kiume,,Fight!!Kumbuka unapigania maisha yako na ya familia yako pia kwa baadaee usikate tamaa!!
 
Apply diploma tu dit pale tabu zote za nini hizo unajitesa mkuu
 
dogo wala usipan bado mapema we tulia soma mambo taratibu tyu utaona yanakaa kichwan yenyewe na uhakikishe kila siku unasoma hatakama hauna mood japo kidogo tyu poa..!
 
soma bila kukata tamaa mambo so magumu bhan jitese hiyo miaka miwil utakula bata mbelen mana kikubwa nikutulia tu..
 
 
komaa na chemistry na maths..phy usihangaike nayo sana
Mkuu PCM aache physics akomae na chem? Course nyingi sana za eng zinataka mtu alie vizuri PH & MT, labda kama anataka kufundisha,

Kama lengo lake kuwa eng akomae sana na PH na maths hyo chem hainaga shida kiivo, but nikuhakikisha physical chem na organic haimsumbui coz hizi topic zinakua na maswali section zote mbili, good enough nasikia siku hizi zile mechanism za kwenye organic walizitoa kwenye syllabus
 
Hamna kombi tamu kama PCM hamna somo rahisi kama PURE MATHS!!! Natamani ningerudi tena advance niendelee kuifurahia maths.
 
Mi binafsi mwanangu hatosoma advance ni kugeana stress tu
 
mdogo angu kama unaweza nenda tabora boys tafuta rafiki kule wa advance fanya mpango hata kupata room. Uwe unasoma na washkaj wa tabora boys. Nawajua warambo wengi sana walikua wanakuja tabora boys na tulikua tunawasaidia tu..na walifaulu vzuri..
 
Kjn mwanaume alie jituma hashindwi
Watu tuliwai pata 7%ya mechanics nusura tukimbilie egm ila tulipo kaza tulichomoka we komaa

Math na chem simple make sure unakuwa nondo kila sector then physics ina wababe wake km sio mbabe choose topic za kukutoa na komaa nazo .utachomoka

Angalizo
Usiwekeze kwenye physics utachinjwa kifo cha boko haram
 
mbona wapo wengi wanao jua physics komaa ww soma kwa kufuata silabasi acha kusolve matango
 
Wengi wamepita huko na walikutana na changamoto hizo, na walifaulu. Hakuna kitu kilicho rahisi, toa muda wako na upambane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…