crms
Member
- Apr 13, 2017
- 18
- 10
Rais wetu tunaomba ulitazame hili kwa jicho pevu. Nakuunga mkono 100% kwa juhudi unazofanya kujenga viwanda, Reli (Standard Gauge, kuziba mianya ya rushwa, kuthibiti mchanga wa madini usisafirishwe nje ya nchi, nk.
Lakini kwa hili la maslahi ya walimu ambao ndio source kubwa ya mafanikio na maendeleo ya nchi hii ya Tz. Walimu ndio wanazalisha madaktari bingwa, engereers, professors, Rais, wabunge, pilots, nk.
Suala la uhakiki wa watumishi ambalo halina ukomo limekwenda sambamba na kutokuboresha maslahi ya watumishi wa umma hasa walimu wale walipandishwa vyeo April 2016 ambao hadi sasa hawajaona mabadiliko kwenye mishahara yao jambo ambalo linafanya walimu waishi kwa matumaini kama vile ni watoto yatima na waliotelekezwa licha ya kauli yako Mheshimiwa Rais ya Mwezi June 2016 kuwa mishahara mipya isitishwe hadi baada ya miezi 2 uhakiki utakapokuwa umekamilika. Je, miezi 2 bado haijaisha?
Naamini kabisa uhakiki wa kina umefanyika kwa kutumia wataalam uliokuwa umewapa hiyo kazi. Kama unavyokumbuka suala la Reli ya Standard Gauge ndivyo tunakuomba uwakumbuke walimu maana mwalimu akitulia kwa mwezi mmoja tu bila kufundisha Taifa linakuwa limepata hasara kubwa mno.
Maisha ni magumu huku uraiani Mh. Rais wetu. Leo hii ukimwomba mtu 200 anakwambia hali ni mbaya sana. Kweli walimu tunaishi kwa matumaini baba.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mimi nakuombea sana nasema kweli maisha ni magumu sana. Watendaji wanasubiri tamko lako Mheshimiwa ili waachie pesa kwenye akaunti za watumishi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais Magufuli