Mahusiano Barabarani. .....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari za mchana,

Nimekuwa na shughuli nyingi kipindi hiki cha kufunga mahesabu ya mwaka kiasi kwamba nakosa muda wa kujiachia kinaga ubaga nikiwa humu, Yaani naingia kwa kuibia kisha narudi kazini.

Kilichonisukuma kuja hapa leo pamoja na kubanwa na kazi ni tukio nililokutana nalo leo. Asubuhi wakati nakuja kazini niko mwenyewe kwenye usafiri na nimefungulia mziki sauti ya kati, mziki unaoimba naupenda vilivyo hivo nikifika eneo la mataa au kwenye foleni basi najikuta aidha napiga makofi au nachezesha mwili kana kwamba nacheza huo mziki husika.

Nikiwa naendelea hivo huku nasuuzika na kutoiona safari ndefu na akili yangu inakuwa imejaa furaha hata nikikutana na stress kazini haziniumizi sana.

Nilifika kwenye moja ya viungia barabara kulikuwa na mataa ya kuongozea magari, ilikuwa sehemu ya kupita magari matata kwa wakati mmoja wote tumesimama tunasubiri mataa yawake tu kanyani pedeli na kuondoka.

Kama kawaida mie nikawa na swing na mziki wangu shingo image uza kichwa upande wa kulia nikaonda ndani ya gari wako watu wawili, mwana mama ndo anaendesha na mwana baba amekaa kiti cha abiria. Wote walikuwa wametizama mbele kama wanasubiria taa iwake waondoke. Nikahisi hawa watakuwa wanandoa, kwanza ni kama wamenuniana, hawaongei hata kidogo na huwa inasemekana ukiona kwenye gari mwanamke na mwanaume kika mmoja anaangalia upande wake au hawaongeleshani au wamenuniana basi hao ni wanandoa. Hasa baba ndo alikuwa sirias kwelikweli....

Nikasema ukute huyu baba hiyo gari ni ya mkewe, yaani mke ndo kakopa kununua gari... ukute mwanaume alikuwa na pesa na magari mwanzoni ila hakulaza mkewe aguse magari yake baadae mwanaume amefilisika mke bado anakipato walau anampa lifti mumewe ila ndo hawaongeleshani. Nikajikuta nawazaa baadae nikajiweka aaaghh hainihusu nikachukua mbele bado taa inawaka nyekundu nikaendelea kuimba na kucheza mziki wangu.

Shingo na kiherehere inanigeuza kichwa upande wa kushoto hapo nikakuta kuna gari inasubiri kukata upande wa kushoto muda wote mie nacheza huku napiga makofi na kuimba wakati huo huo nawaza alikuwa akinitizama. Nikipogeuka kumtazama tukakutana uso kwa uso, tukajikuta wote tume tabasamu huyu kaka nae alikuwa mwenyewe kwenye gari.

Haikuchukua hata sekunde tatu taa zikaruhusu kuondoka. Sasa mie nikajikuta nacheka zaidi maana yeye kumbe muda wote ananitizama ni kama anasema eeh wee dada unapenda kuimba na kucheza.....

Baada ya pale akili ikaniambia. .....

Kasie kwanini watu wakiwa kwenye mahusiano wanalala chumba na kitanda kimoja wakitoka nje wanaonekana wazi hakuna mawasiliano au mahusiano mazuri?

Mie niko singo na huwa nakuwa na stress zangu lakini hata nikinuniana na mtu kwenye gari nakuwa nakula mziki happy day, happy Kasie.

Yule mkaka nahisi atakuwa kaoa ila kwakuwa hakuwa na mkewe kwenye gari pengine akaweza kutabasamu hata kama aligombana na mkewe nyumbani. Ila kama angekuwa na mkewe kwanza asingeweza kunichekea siajabu nae angekuwa amenuna.

Hivi kwanini wenye mahusiano ya ndoa huwa wananuniana kwenye gari? Mie hata kama usafiri ndo huo mmoja bora nipande zangu daladala kuliko kwenda njia nzima kimyaa, kwanza nnavopenda kuimba ningekuwa na mume angesema nampigia kelele.

Pia najiuliza kwanini ni rahisi sana kwangu kuwa na mahusiano mapya barabarani. .... siku hizi nimeacha tuu kuyaripoti ila yako mengii.

Kama mmoja wiki iliyopita alinipita kwa speeds akiwa anaendesha mark X halafu nikaja kumkera mbele kasimama amewasha taa za hazard. Akanisimamisha kuomba msaada nikasimama akanifata na kuelezea shida yake.... nikamjibu kiutani mbio zote zile kumbe unakwama mbele tu kachoka wote, hadi leo hii tu marafiki.

Huyo ndo Kasie na mahusiano barabarani, narudi kazini sasa baadae.

Kasie Matata Mahaba.
 

Hey Kasiba....

Ulikuwa unasikiliza wimbo gani? Kamata chini?
 
mie mwenyewe ni michuno tu,leo nimetoka bunju hadi city centre sijafungua mdomo kuongea na wife
 
Mkuu Kasie mahusiano yanakuwa na siri nyingi mnoo. Siri ni mmoja kujishusha tu baas, wengi hawaelewi hili na ndio maana maogomvi hayaishi kibaya zaidi mbele ya watoto, watoto wanakuwa mwisho wa siku watoto wetu ndio hivyo wanaenda kuoa nje ya nchi utadhani ndani hakuna wadada.
 
Hey Kasiba....

Ulikuwa unasikiliza wimbo gani? Kamata chini?

Juujuu man. ...... aahahahhahahahahaaa

Nilikuwa nasikikiza wimbo unaimbwa. ....

Amenipa Juujuu ooh ooh ooh
Amenipa Juujuu .... ...... .....

Sijui nani ndo kauimba huo wimbo.
 
Kasie njoo nikuoe

Hahahahaaa looh dadiiiiii akikupa kibali nakuja mzima mzima hehehehe.

Ila usiache nikapoteza tabasamu langu na kuanza kununa njia nzima.

Smile is the dress Kasie wears everyday.
 
mie mwenyewe ni michuno tu,leo nimetoka bunju hadi city centre sijafungua mdomo kuongea na wife

Duuh yaani mie kwakweli hayo manuno sitaweza hata kidogo. Napenda vichekesho napenda kucheka napenda kuimba napenda kutabasamu. Bora kila mmoja atumie usafiri wake jioni mnasimuliana.

Pole aiseeh.
 

Sasa hizo siri ndo kununiana utasema maadui aiiihh. ...


Shangaa sasa mtu na mchepuko wake kwenye gari hadi mafenesi na zabibu wanalishana kwenye gari....na kutekenyana juu...
 
Kabisaaa, furahini muongeze siku za kuishi.

Kununa husababishwa na maugomvi au makwazo na kuendelea kununa ni chanzo cha maugomvi mengine.

I enjoy being alone..... All by myself.
Kwakweli nitaanza karibuni
 
Juujuu man. ...... aahahahhahahahahaaa

Nilikuwa nasikikiza wimbo unaimbwa. ....

Amenipa Juujuu ooh ooh ooh
Amenipa Juujuu .... ...... .....

Sijui nani ndo kauimba huo wimbo.
Kaimba Nameless, mume wa Wahuu.
 
Sasa hizo siri ndo kununiana utasema maadui aiiihh. ...


Shangaa sasa mtu na mchepuko wake kwenye gari hadi mafenesi na zabibu wanalishana kwenye gari....na kutekenyana juu...

Aiseeee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…