Mahubiri ndani ya mabasi ya mwendo kasi ni kero

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Kumezuka Tabia ya baadhi ya watu kuanza kutoa mahubiri ya dini katika mabasi ya mwendokasi.

Ukweli sio sahihi kufanya hivyo kwani kuna watu ambao hawako tayari kuyasikiliza Kwa hiyo wanalazimishwa.

Nadhani mahubiri ya sehemu zake hebu tuyaache mabasi ya mwendokasi yafanye Kazi zake.Tunauomba uongozi wa DART upige marufuku mahubiri ya dini yoyote katikamabasi yake
 
Wewe mleta mada dini gani??
Hiyo ni isue ya opportunity, ukiona itumie nadhani jamaa wameona opportunity wanaitumia kwa sababu ya uwingi wa watu. kwa kawaida wanadamu hawapendi kusikia kweli hivyo mahubiri mara nyingi yahazipendezi nafasi nyingi, hasa ukizingatia umetoka umepiga mahali alfu jamaa anakupigia neno acha ukatubu ni dhambi.

bilashaka kukubaliana naye ni ngumu, lakini pia watu wanahisi wamechoka na hawaitaji kutafakari kitu kingine, japo kimsingi hapo ndipo maarifa hutoka Mungu hutoa maarifa kwa watu toka kwake.

chamsingi watoa hizo maada wawe na hekima na kujua wanaongea na watu waliochoka kimawazo na wanaitaji kuambia kwa urafiki fulani unaovutia usikilizaji.
 
Halafu wakimaliza wanakusanya sadaka,aiseee
Hivi wanalipa nauli kweli wale jamaa?
Ila inakera kila kitu kina sehem zake,mbona mitaani kwao hawapiti
Unaamka unamuona akimaka mbio Ubungo au Stand kwakujua kwamba kuna hela,lakini mtaani kwake hata siku moja hajasema apite house to house.Nasubiri niwaone kwenye ndege,hahahaha au nauli msala
Halafu kama wamekariri hawa jamaa,unaweza kukuta kila ukipanda maudhui yale yale ambapo hata mie naweza,maana hakuna maswali pale
 
Ibada ni jambo jema. Lakini pale haya mabasi yaendayo kasi yanapogeuka kuwa sehemu ya ibada muda wote inaweza kuwa kero kwa wengine ukizingatia kwamba kwenye huo usafiri kunakuwa na watu wenye imani tofauti. Na pia inakuwa kama vile kuhubiria watu kwa lazima kwa sababu abiria wanakuwa hawana namna ya kutosikiliza mahubiri hayo kwa asilimia mia moja. Hii ni tofauti na kwenye nyumba za ibada au mihadhara/ mahubiri inayofanyika kwenye maeneo maalumu ambapo anaekwenda au kusimama eneo hilo anakuwa ameshajiandaa kusikiliza neno la uzima. Ni vizuri suala hili likaangaliwa kwa karibu ili kuepusha usumbufu kwa watumiaji wa aina zote wa usafiri huo.
 
kuhubiliwa lazima muhubiliwe ndugu,.mtake msitake,kuokoka ndo mtachagua sasa,hulazimishwi kuokoka ila ni hiari yako binafsi.akina petro walifungwa gerezani,.kwaa ajili ya jina la YESU, Na YESU mwenyewe walimchukia injili yake kwa aliwachoma mioyo washika dini na wafia dini wasiompenda MUNGU,ila walipenda uponyaji wake na nguvu zake,.ila YESU alihubiri hadi wakamuua kwa mateso makali ya kumsulibisha msalabani,.so wewe ndugu injili utaisikiA tu ili uache dhambi,maana mtu anaechukia injili ni yule ambaye anachomwa na ukweli neno,kuwa anaambiwa uache dhambi,amwamini YESU,.so injili itahubiliwa kwa njia yoyote tu,hata damu ikimwagika kwa kuua wahubiri,..YESU atahubiliwa,.stefano alikufa kwa kupigwa mawe,.aya waliomuua leo wapo?????????ndugu badili njia zako upende injili
mathayo 24;14
tena habari njema ya ufalme itahubiliwa katika ulimwengu wote,kuwa ushuhuda kwa mataifa yote;hapo ndipo ule mwisho utakapokuja,..
mathayo 10;22-23
22;nanyi(WAHUBIRI) mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu(jina la YESU)..........


ndugu lazima huubiliwe yani hata kama hutaki ili hukumu iwe ya haki juu yako.
kumbuka nuhu alitengeneza safina hadharani tu,sio mafichoni na watu wakamdhihaki sana,.ila nuhu alisimama katika kweli na kuhubili kuwa watu acheni dhambi mtaangamia,.ila watu kama leo wakawa wabishi........
injili itahubiliwa hata humu jf ili ubadilike
 
Back
Top Bottom