Hapana,
Moja ya mila ni kwamba ukitaka kuoa mambo yote yanapitia kwa washenga.
Kikwelikweli kwa utamaduni wetu hata hutakiwi kumjua kwa sana personally mke mtarajiwa, kuna watu maalum kazi yao kumchunguza na ku negotiate mahari.
Sio siku hizi watu mshakaa, mshatiana mimba, mshazichoropoa (ashakum, ndo ukweli wenyewe), leo mnaenda kuulizana mahari?
Au binti hata litmus test ya Tantawi hawezi kupita hana hata haya anadai mahari na yeye!
La!
Mahari si lazima uimalize, ulizia kabila lao mila zikoje.
Unaweza kutoa "kishikia mke" ukachukua mke wako, mahari iliyobakia ukaweka kwenye "college fund" ya wanenu.Nyingine utawafadhili wazee vitu vidogovidogo over the years ambayo itakuja kuwa zaidi ya mahari.
Pengine unatajiwa kupimwa uanaume wako na nia tu.
Kutishika kwa kitu kama bei wakati hujaanza ku bargain si biashara.
Yeah, biashara, maana ishakuwa biashara siku hizi.
Tunahamia kwetu na wote tunakuwa vichwa vya familia. Kuna ubaya hapo?
Usawa huu hamna kuoa babake.
Kweli aisee ila tatizo na hizi mila zetu siku ambayo umekuwa babu mke wako akifariki unaambiwa umalizie mahari kwanza ndi ukazike na wanakomaa kweli
Duuh,
Hii noma mazee, inabidi uwe mdogo tu hapo.
Hizi mila unaweza kukamilisha mahari, unataka kuchukua mke kuna kibabu kinatokea kinadai hakijapata usinga wake.
Inabidi kukohoa tu kama ndo ushakubali mila hizi.
Oa usiogope Kiranga, hapo wanaweza kuanza 4 million mwisho wa siku wakafikia muafaka laki 8 na bado jamaa akatoa laki 4 na ndoa ikafanyika. Kwa familia zinazoelewa mahari ni utaratibu ambao umewekwa na mababu zetu wanakuwa wanaundeleza kama sehemu ya kukamilisha mila na desturi hata kama wahusika na wazazi wamekulia mjini
juzi juzi mdogo wangu kaolewa, tunaenda kupanga mahari, wazee wanasema ng'ombe 5 kila ng'ombe 100,000; mbuzi 10, kila mbuzi 20,000; mi nikabaki nashangaa tu....... tukawa tunakonyezana na mdogo wangu hapa tutaiskia kuku kwa 1,000.inaweza kuwa hivyo.
Bei ya ng'ombe wa mahari huwa sio kama anavyouzwa sokoni, anakuwa na bei ya chini zaidi.
Hii huwa naona tunavyobargain wakati wa mahari.
Sasa hapa kama ng'ombe sokoni ni laki mbili kwa msimu huu wa kiangazi, basi ng'ombe wa mahari anaweza thamanishwa kati ya 125,000 hadi 150,000.
juzi juzi mdogo wangu kaolewa, tunaenda kupanga mahari, wazee wanasema ng'ombe 5 kila ng'ombe 100,000; mbuzi 10, kila mbuzi 20,000; mi nikabaki nashangaa tu....... tukawa tunakonyezana na mdogo wangu hapa tutaiskia kuku kwa 1,000.