Mahakama ya mafisadi kuanza Julai, 2016. Ofisi za AG, DPP kuimarishwa kuharakisha kesi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Tamko la kuanza kazi kwa Mahakama hiyo lilitolewa jana bungeni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi yake.

“Kuhusu ahadi ya kuanzisha Mahakama Maalum ya Ufisadi napenda kuliarifu Bunge lako kwamba, Serikali imeanzisha Divisheni ya Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi mwezi Julai 2016,” alisema Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu alisema pia Serikali itaimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki kwa kesi zitakazofikishwa kwenye mahakama hiyo.

Kiongozi huyo wa serikali aliongeza: "Serikali itaimarisha ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kwa pamoja ziweze kuharakisha utoaji wa haki."

Rais Magufuli alitoa ahadi ya kuanzisha mahakama hiyo kwenye mikoa kadhaa aliyopita kwa ajili ya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Aidha, katika siku ya kilele cha Wiki ya Mwaka Mpya wa Mahakama Jijini Dar es salaam mapema mwaka huu, Rais Magufuli alimtaka Jaji Mkuu, Othman Chande kutosubiri Bunge kupitisha Sheria ya Uanzishwaji wa Mahakama ya Mafasidi, badala yake mahakama hiyo ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.

Alisema kuchelewesha kuanza kwa mahakama hiyo kunatoa mwanya kwa mafisadi kuendelea kuangamiza nchi na kuifanya kuwa masikini wakati ina rasilimali za kutosha ambazo zinaweza kuiendesha nchi bila kutegemea fedha za wafadhili.

Rais Magufuli alisisitiza umuhimu wa uanzishwaji wa mahakama hiyo ambayo alitaka ifanye kazi ndani ya mahakama kuu kama zilivyo Mahakama za Ardhi na Biashara.

Akifunga maadhimisho hayo, Rais Magufuli alisema azma yake ni kuona nchi inakuwa na uchumi mzuri ambao utamnufaisha kila mtanzania na rasilimali zilizopo badala ya kumilikiwa na watu wachache.

SH. BILIONI 12.3

Akizungumza Bungeni jana, Majaliwa alisema katika jitihada za kukabiliana na changamoto ya uhaba wa majengo ya mahakama na vitendea kazi katika ngazi zote, Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake aliyoitoa Februari 4, mwaka huu ya kutoa fedha za maendeleo ya mahakama Sh. bilioni 12.3.

Alisema hatua hiyo imewezesha mahakama kuendelea na ukarabati na ujenzi wa mahakama katika ngazi mbalimbali pamoja na ununuzi wa vitendea kazi.

Majaliwa alisema serikali imedhamiria kupunguza kero ya mlundikano wa mashauri mahakamani ili wananchi wapate haki kwa wakati.

Katika kufanikisha dhamira hiyo, Waziri Mkuu alisema serikali imeimarisha utendaji wa mhimili wa mahakama kwa kuongeza rasilimali watu na fedha.

"Serikali pia imeboresha na kuongeza ufanisi katika upelelezi na uendeshaji wa mashauri kwa kutenganisha jukumu la upelelezi na uendeshaji mashuari,” alisema Majaliwa.

Uongozi wa mahakama, alisema zaidi Majaliwa, umejiwekea utaratibu wa majaji na mahakimu kuwa na malengo ya idadi ya mashauri ambayo wanapaswa kuyasikiliza kila mwaka.


Chanzo: Nipashe
 
Hapa kama nikisasi mahakama hiyo itadhihirisha. Na tunahasira nao hao waliokuwa wakiigeuza nchi kama benki bubu zao. Kwa kisasi hiki naunga mkono
 
Mdogomdogo tunakuja kwa mzee wa richmond
Ni kweli kabisa, bila kusahau EPA, MEREMETA, KAGODA, KIWILA COAL MINE, RADAR, IPTL, ESCROW, LUGUMI, DARAJA LA DAU, MABEHEWA FEKI, KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM, UDA, ...
 
Mahakama ya mafisadi kwa sheria zilezile! Waseme wameongeza vyumba vya mahakama tui

Na Sheria zile zile zimeshindwa kutoa matokeo tuliyo yatarajia iwe kwa kuchelewa au kwa wakati ,pesa zetu zoote walizokwiba Mafisadi nchi hii hatujarudisha hata senti tano sana sana tumeushia kukimbizana na masikini mtaani huku na kuwanyang'anya magari kama 'Pic up' huku tukishangilia kuwa tunapambana na mafisadi....Maigizo plus plus yana tuchosha ...
 
Huwezi kufurahia utekelezaji,umezoea blah blah....kuna mambo ni bora ukae kimya.
Hakuna cha utekelezaji zaidi ya kuwagelesha watanzania tu, kama upo na ufahamu wako vizuri jiulize kwanini katiba pendekezwa ya wananchi ilipigwa chini?
Otherwise endelea kuuza mashati ya chama hapo Lumumba.
 
Nahisi wataonewa wengi sana na hilo limahakama lao.. Kama watakuwa siriaz waanze na mh Mkapa kwa kufanya biashara ikulu... Mh Kikwete Trion 4 safari za nje.. Mh Mwakyembe mabehewa fake.. Mh Magufuli kuuza nyumba za Umma
 
Ulipo tupo hawatamani kabisa kusikia kitu kinachoitwa mahakama ya mafisadi. Wanahofu kipenzi chao anaweza kuozea jela.
 
Back
Top Bottom